Get Program kurudi upya WPL

KOCHA wa Get Program iliyopanda daraja msimu huu, Aristides Ngowi licha ya kuwa na wachezaji wengi vijana ambao hawana uzoefu na ligi, lakini wanapambana jambo linalowapa motisha ya kujipanga upya kipindi hiki cha mapumziko.

Timu hiyo haikuanza vyema ligi ikipitia changamoto ya ukata uliosababisha baadhi ya wachezaji kutimka kambini na kutafuta changamoto sehemu mbalimbali.

Wachezaji hao ni pamoja na Zubeda Mgunda, Diana Mnally, Protasia Mbunda waliotimka Yanga Princess na Zainabu Mohamed aliyetimkia Mashujaa Queens.

Ngowi alisema kama kocha anapambana na mabinti wadogo ambao wengi wamesajili kutoka Ligi ya Mkoa ambao bado hawana uzoefu na ligi akiamini wakipata muda kidogo watakuwa bora.

Aliongeza wanapaswa kukaza buti kwenye mechi zilizosalia ili kuhakikisha timu hairudi Ligi Daraja la Kwanza ikiwemo kushinda karibu kila mchezo.

“Vijana bado wadogo, hata hivyo wanajitahidi sana, tumepitia kipindi kigumu hapa kati lakini wanapambana sana, mipango ni kubaki Ligi Kuu na si kingine,” alisema Ngowi.

Related Posts