NA WILLIUM PAUL, MOSHI.
MKUU wa mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu amesema kuwa wapo baadhi ya Wananchi wamekuwa wakitumia fedha ya Jamuhuri vibaya huku wengine wakiwa na mitambo ya kuiibia Serikali na Wananchi na kuipongeza Wizara ya Fedha kupitia Hazina kuona umuhimu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya fedha.
Babu alitoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipokutana na timu maalum kutoka Hazina ambayo itaweka kambi ya siku 14 mkoani Kilimanjaro kutoa elimu ya matumizi sahihi ya fedha ambapo alisema kuwa, kupitia elimu hiyo ambayo itayafikia makundi mbalimbali itasaidia wananchi kutambua matumizi sahihi ya fedha.
“Nimefurahi kusikia mtafika katika shule za msingi na sekondari mtawasaidia vijana kwa sababu wapo vijana hawatambui thamani ya fedha ile noti ya elfu kumi au elfu tano utaikuta inafanyiwa kitu cha ajabu hivyo mkiwaelimisha itasaidia sana” alisema Babu.
Na kuongeza “ wapo watu wanatumia fedha yetu ya Jamuhuri vibaya na wengine wanamitambo ya kuiibia serikali na Wananchi kupitia elimu hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza na kumaliza kabisa tatizo hili” alisema Dionisia alisema kuwa watatoa elimu ya uwekaji akiba, utoaji wa mikopo uwekezaji na mpango wa kustaafu lengo likiwa ni kuwahamasisha wananchi kutumia huduma sahihi za fedha ambazo zinasimamia na mamlaka ya usimizi wa fedha.
“Lengo jingine ni kuhamasisha wananchi waweze kupanga mapato na matumizi ya fedha zao ili kuhakikisha wanakuwa na maendeleo katika familia na uchumi kwa ujumla pamoja na kuhakikisha wanakopa katika taasisi zenye riba sahihi na sio taasisi zinazochaji riba kubwa”.