Wawili wafariki dunia ajali Handeni, yumo askari JWTZ

Watu wawili wamefariki dunia katika ajali ya gari iliyohusisha Toyota Noah kuigonga Toyota Canter ambayo ilikuwa pembeni ya barabara usiku wa kuamkia leo Jumatatu Januari 10, 2025 katika eneo la Kauzeni, Kata ya Kwenjugo wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga.

Akizungumza na Mwananchi Digital leo asubuhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema Noah iliyokuwa inatoka barabara ya Korogwe kwenda Handeni ilipofika eneo la Kauzeni kwenye kona ilimshinda dereva na alikuwa na mwendo mkali na kwenda kuigonga Canter.

Amesema abiria kadhaa waliokuwa kwenye Noah hiyo walipata majeraha ambapo walipelekwa Hospitali ya Mji Handeni pamoja na miili ya marehemu imehifadhiwa kwa ajili ya taratibu nyingine.

Katika taarifa yake aliyoitoa kwa umma kupitia makundi ya WhatssApp Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Albert Msando amesema kati ya waliofariki kwenye ajali yupo askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kutoka  Kikosi cha 83 Vigwaza aliyefahamika kwa jina la Abdul Kareem Kimemeneke (49) ambaye ni mkazi wa Kwamfuko  Kata ya Vibaoni, Handeni.
Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi

Related Posts