Mayele ni rekodi juu ya rekodi Misri

Oktoba 3, 2024, Fiston Mayele alipiga pasi mbili za mwisho dhidi ya El Dakhlia ambazo zilichangia kuiwezesha Pyramids FC kupata ushindi wa mabao 2-0 na zikamfanya afikie rekodi moja tamu kwenye Ligi Kuu ya Misri.

Pasi hizo mbili zilimfanya afikie rekodi ya Kabongo Kasongo ya kuwa raia wa DR Congo aliyepiga pasi nyingi za mwisho kwenye ligi hiyo.

Mayele alifikisha pasi sita za mwisho ambazo zilimfanya awe sawa na Kabongo na hivyo sasa anatafuta angalau moja tu ili aongoze chati ya nyota wa DR Congo waliopiga pasi nyingi za mwisho kwenye ligi hiyo.

Wakati Mayele akimfikia Kasongo kwenye upigaji pasi za mwisho, nyota huyo wa Yanga, katika mechi 12 zilizopita za Ligi Kuu ya Misri amefunga mabao matano yanayomfanya ashike nafasi ya tatu katika chati ya kufumania nyavu msimu huu nyuma ya Emmam Ashor wa Al Ahly mwenye mabao saba, Nasser Amr wa Pharco na Nasser Mansy wa Zamalek.

Hata hivyo mabao hayo matano yamemfanya afikie na kuvunja rekodi iliyowahi kuwekwa na Kabongo Kasongo ya kuwa Mcongo aliyefunga idadi kubwa ya mabao katika Ligi Kuu ya Misri.

Kasongo ambaye aliwahi kuzichezea Zamalek na Al Ittihad alifunga idadi ya mabao 28 katika mechi 81 za ligi hiyo.

Hata hivyo timu zikiwa zimecheza mechi 12 msimu huu, Mayele mabao yake matano yamefanya afikishe idadi ya mabao 30 ambayo yanamfanya awe mbele ya Kasongo kwa mabao mawili zaidi.

Safari ya Mayele kuvunja rekodi hiyo ilianzia katika mechi dhidi ya Petrojet Novemba Mosi mwaka jana akifunga bao moja kisha akafunga dhidi ya Pharco, Disemba 25, 2024.

Januari 15, 2015 akafunga bao dhidi ya El Mehalla na Januari 22 mwaka huu akapachika bao moja dhidi ya Zed FC.

Katika mchezo dhidi ya Zamalek, Januari 31 mwaka huu akapachika bao lingine moja ndipo akajihakikishia rekodi yake hiyo kwa mabao mawili zaidi

Related Posts