Mkongwe Mangwana Aachia Albam Uzeeni – Global Publishers

mwanamuziki mashuhuri wa muziki wa dansi wa rhumba ya Kikongo, Sam Mangwana

Sam Mangwana (80) ni mwanamuziki mashuhuri wa muziki wa dansi wa rhumba ya Kikongo, ambaye ni mwimbaji kutoka Angola, ameifanya Afrika iendelee kucheza rhumba kwa zaidi ya nusu karne.
Albamu yake mpya, Lubamba, ni ushuhuda wa mapenzi yake yasiyoyumba kwa muziki na kipaji chake cha kudumu.

Baada ya miaka sitini ya taaluma, mtunzi huyu mahiri bado anaendelea kung’ara katika muziki. Akiwa na mtazamo wenye kung’aa, sauti tulivu, nzito na yenye ukarimu, gwiji huyu wa rhumba ya Kikongo – ambayo aliipanua kwa sauti nyingine tofauti – anawasilisha albamu yake Lubamba nchini Ufaransa.

Akiimba kwa Kikongo, Lingala, Kifaransa au Kireno, nyimbo zake daima hubeba alama yake ya kipekee, zikiunganisha miondoko ya nchi za Kiafrika zinazozungumza Kireno pamoja na mitindo inayotikisa kiuno ya muziki wa Amerika ya Kusini na Karibea.

Alizaliwa mwaka 1945 jijini Kinshasa (wakati huo ikiitwa Leopoldville), Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kwa wazazi wa Angola. Amesafiri pembe zote za Afrika, pamoja na Marekani na Ulaya, ambako kipaji chake kimeangaza.

Alianza kung’ara akiwa na umri wa miaka 18 katika bendi ya African Fiesta ya Tabu Ley Rochereau, kisha akaungana na OK Jazz ya Franco. Baadaye alishirikiana kuanzisha makundi kama Festival des Maquisards na African All Stars huko Abidjan. Isikilize Lubamba, utaamini ujuzi hauzeeki. Wimbo huu uliobeba albamu aliutunga mwaka juzi.

Related Posts