Na Rahma Khamis Maelezo
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi
amesema Serikali itaendelea kuweka misingi Bora ya Haki ili wananchi
kupata haki zao.
Ameyasema hayo Uwanja wa Mahakama ya Mkoa Mazizini Wilaya ya Magharibi ‘B’ katika kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Sheria.
Amesema uwepo wa Sheria na upatikanaji wa Haki ni jambo muhimu kwani itawawezesha wananchi kupata mafanikio
Rais Mwinyi amezisisitiza mahkama kutumia maadili katika kazi zao ili wananchi wapate nafasi ya kusema yale waliyonayo.
Aidha
amesema kuwa maboresho ya Sheria lazima yaende sambamba na upatikanaji
wa haki kwa wakati hivyo ni vyema kuweka utaratibu mzuri na mwepesi ili
kuwarahisishia wananchi.
Nae
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba,Sheria, Utumishi na Utawala Bora
Dkt Haruon Ali Suleiman amewataka majaji na mahakimu kujitahidi katika
utendaji wa kazi zao ili kesi zisichukue muda mrefu.
Akitoa
salamu Jaji Mkuu wa Zanzibar Khamis Ramadhan Abdalla amesema kufanyika
kwa maadhimisho hayo kunaashiria kumalizika kwa mapumziko ya mahakama
na kuukaribisha mwaka mpya wa shughuli za mahakama.
Amesema
kuwa maadhimisho hayo kwa Zanzibar ni ya kumi na nne ambapo Kauli mbiu
yake inaunga mkono uimarishaji wa misingi ya haki na sheria pamoja na
kuitaka jamii na Taasisi mbali mbali kufahamu kuwa mahakama ndio
kimbilio la upatikanaji wa Haki.
Aidha
amefahamisha kuwa kwa mwaka 2024 vikao 224 vilifanyika na kushirikisha
Watendaji mbalimbali ikiwemo Mkemia Mkuu wa Serikali, Afisi ya
Mwanansheria Mkuu pamoja na utungaji wa Sheria ya mahakama ya mwaka 2023
ya mahkama ya kadhi ili kurahisisha upatikanaji wa Haki.
Mwanansheria
Mkuu wa Zanzibar Mwinyi Talib Haji ameipongeza Serikali ya awamu ya
nane kwa kuweka na kuimarisha miundombinu ya Sheria kwa kuweka misingi
imara ya upatikanaji wa ikiwemo vitendea kazi na watendaji wake.
Aidha
amefahamisha kuwa Afisi imekamilisha mapitio ya Sheria mpya hivyo
itarahisisha upatikanaji wa Sheria pamoja na kukamilisha rasimu ya
Sheria na baadae kupitisha katika Baraza la Wawakilishi.
Maadhimisho
ya Sheria hufanyika kila mwaka ambapo Kaulimbiu ya mwaka huu Utawala wa
Sheria ndio Msingi wa Haki,Amani na maendeleo katika jamii.