WANUFAIKA WA MIKOPO YA ELIMU YA JUU WATAMBUE KUWA WANADENI – MTAMBULE

Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Saad Mtambule akipokea jezi kwaajili ya mbio za hisani zitakazofanyika jijini Dar es Salaam kutoka kwa Kaimu Meneja wa Kanda ya mashariki (HESLB) Ramadhani Ndongwala.

Kaimu Meneja wa Kanda ya mashariki (HESLB) Ramadhani Ndongwala akizungumza na waandishi wa habari juu ya miaka 20 ya Bodi ya mikopo hapa nchini.

Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Saad Mtambule akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea mabanda katika maadhimisho ya miaka 20 ya bodi ya mikopo.

Picha ya pamoja na wafanyakazi wa bodi ya mikopo.

Mkuu wa wilaya ya kinondoni, Saad Mtambule akipita katika mambanda mbalimbali kwaajili ya kusikiliza huduma wanazotoa.

Na Avila Kakingo, Michuzi Tv

MKUU wa wilaya ya kinondoni, Saad Mtambule amesema kama vyuo, wazazi, walezi na waajiri watasimamia vizuri wanafunzi ambao ni wanufaika wa mikopo kurudisha mikopo wa wakati taifa litapata wahitimu wenye tija.

Hayo yamesemwa leo Februari 13, 2025 jijini Dar es salaam kwenye Maaadhimisho ya miaka 20 ya Bodi ya mikopo yanayoendelea kufanyika katika kanda mbalimbali ambapo waajiri wa vyuo na taasisi mbalimbali Tanzania amewataka kutoa ushirikiano kwa Bodi ya Mikopo Nchini (HESLB), kuwafichua wadaiwa na kusimamia vizuri wanafunzi ili kupata zao ambalo litakalorudisha mikopo baada ya kuhitimu.

Pia amewasisitiza wahitimu wa elimu ya juu kutambua kuwa wanapohitimu watambue kuwa wana deni walioacha hivyo kuwa waamini kwa kurejesha mikopo kwa wakati ili kuweza kuwanufaisha kizazi kingine.

Hata hivyo Dc Saad amewataka watanzania kujitokeza katika viwanja vya Biafra kinondoni kuweza kupata huduma zinazotolewa katika maaadhimisho ya miaka 20 ya HESLB.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Kanda ya mashariki (HESLB) Ramadhani Ndongwala amesema katika kuadhimisha miaka 20 ya Bodi hiyo tangu kuanzishwa kwakwe 2004 inashererekea kwa kuandaa maonesho ya katika kanda tofauti hapa nchini pamoja na kuandaa matembezi ya hisani yatakayofanyika katika viwanja vya farasi Oysterbay Dar es Salaam.

Hata hivyo amesema kiwango Cha fedha kilichotolewa na serikali kimeongezeka wakati huu chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ukilinganisha na awamu zilizopita hivyo kufanya wanuafaika wengi kuweza kunuifaka na Mikopo ya elimu ya juu pamoja na pesa ya chakula na malazi kutoka sh. 8500 hadi sh. 10,000 kwa siku.

Hata hivyo Ndongwala amewaomba wazazi , walezi, wanachuo kuzingatia maelekezo ambayo yametolewa na HESLB ili waweze kujaza fomu kwa usahihi zaidi pale wanapoomba mikopo ili kila mmoja anufaike na fursa inayotolewa na serikali.

Amesema katika miaka 20 ya HESLB wanajivunia kutoa huduma zuri na bora kwa mpaka sasa washatoa mikopo ya sh. Trioni nane kwa wanafunzi zaidi ya laki nane.

“Tunajivunia tumetoa mikopo kwa watanzania wengi wenye hali za chini ambao bila bodi ya mikopo pengine wasingeweza kusoma vyuo vya elimu ya juu.” Amesema Ndongwala

Pamoja na mambo mengine Dc, Mbambule alitembelea mabanda yote katika maonesho hayo yaliyoandaliwa kwaajili ya kuadhimisha miaka 20 ya HESLB.

Related Posts