Ukiwa na cheo hautakiwi kuwa mchoyo kwa wenzako
Ni Moja ya nukuu ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa (NEC) wa Mkoa wa Mbeya Ndugu Ndele Jailos Mwaselela akitekeleza Ahadi yake leo Februari 15, 2025 ya kuchangia ukarabati wa ofisi 32 za chama hicho Mbeya Vijijini.
Katika Wilaya hiyo, M-NEC Ndele Mwaselela amechangia zaidi ya Shilingi Milioni 30 ambapo leo ametoa Shilingi Laki Saba (700,000) kwa kila Kata za chama hicho.
Makabidhiano ya fedha hizo yamefanyika katika Ukumbi wa shule ya Mbalizi High School mbele ya viongozi wa chama hicho Kata zote 32.
Katika hotuba yake amewasihi viongozi kuacha malumbano kwa kusema kuwa Malumbano yao hayawasaidii wananchi.
Huku akinukuu hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa Tarehe 7-8/12/2022 hasa suala la viongozi kuwajibika na kwamba kila kiongozi anatakiwa kujihoji kuwa je anakimbiliwa na wananchi au anakimbiwa? Na kwamba sifa ya kiongozi ni kutetea watu.
Aidha amewasihi viongozi hao kutochukia wanapokosolewa “Natoa wito wa kukosoana bila kuchukiana” amesema M-NEC Mwaselela.
Pia alienda mbali zaidi akinukuu kitabu kisichopendwa na viongozi wengi kilichoandikwa na Mwalimu Julius Nyerere kiitwacho TUJISAHIHIAHE akijielekeza ukurasa wa 18-19 kinachosisitiza viongozi kuwasikiliza watu.
Amesema kufika Mwaka 2026 atahakikisha amechangia ofisi zote za chama hicho katika Mkoa wa Mbeya.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mbeya Vijijini ndugu Akimu Sebastian Mwalupindi baada ya kupokea mchango wa M-NEC Ndele Mwaselela, amemshukuru na kusema kwamba kwasababu chama kinajengwa na wanachama wote, anakaribisha wachangiaji wengine huku akisisitiza kufuata taratibu za chama kama alivyofanya M-NEC huyo.
Pia amewasisitiza viongozi wa Kata zote kwenda kutumia fedha hizo katika malengo husika.