MKURUGENZI MOSHI ATOKWA MACHOZI, CCM NA CHADEMA WAKIMPA ZAWADI .


Mkurugenzi wa Halmashauriya Manispaa ya Moshi Mwajuma NAsombe akizungumza wakati wa kikao cha mwisho cha Bajeti cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri .

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo akizungumza jambo katika kikao hicho ,kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe .

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi wakikabidhi keki kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe kama zawadi kutokana na namna alivyosimamia manispaa hiyo pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo kufanikisha kupaa kwa mapato ya halmashauri.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe akipokea zawadi ya seti ya vyombo kwa ajili ya chakula kutoka kwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Moshi kutokana na namna alivyosimamia manispaa hiyo pamoja na watendaji wa halmashauri hiyo kufanikisha kupaa kwa mapato ya halmashauri.


Diwani wa kata ya Kiboriloni Frank Kagoma (Chadema) akiwaamebeba zawadi ya jagi la kuchemshia chai ikiwa ni zawadi aliyotoa kwa mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi kutokana na utendajikazi wake .
Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe akifurahia zawadi ya JAgi alilopewa na Diwani wa kata ya Kiboriloni Frank Kagoma (Chadema) kama zawadi .

Na Dixon Hussein – Moshi

Katika hatua isiyo ya kawaida katika siasa za Tanzania, diwani pekee wa upinzani katika baraza la madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi Frank Kagoma (Chadema) ameungana na Chama cha Mapinduzi (CCM) kutoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi kwa usimamizi thabiti wa mapato na miradi ya maendeleo.

Mh Kagoma ambaye ni diwani wa kata ya Kiboriloni na viongozi wa CCM wilaya ya Moshi wametoa pongezi hizo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika mjini Moshi, ambapo viongozi wa halmashauri hiyo walitangaza ongezeko kubwa la mapato kutoka bilioni 41.7 hadi bilioni 53.2 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/24.

Katika kikao hicho,Mh Kagoma amekiri kuwa licha ya tofauti za kisiasa, hawezi kupuuza ukweli kwamba usimamizi mzuri wa halmashauri umeleta matokeo chanya kwa wananchi wa Moshi.

“Mimi ni mpinzani lakini siwezi kupinga maendeleo yanayoonekana. Tumeona miradi ya halmashauri ikitekelezwa kwa wakati, mapato yakiongezeka,hii ni hatua nzuri kwa wananchi,” alisema.

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi wakiongozwa na Mwenyekiti wake Faraji Swai pamoja na Madiwani wa CCM wameonyesha furaha yao kwa ufanisi huo, wakisema kuwa halmashauri inatekeleza kwa vitendo ilani ya chama chao kwa kuhakikisha rasilimali zinatumika ipasavyo kwa maendeleo ya wananchi.

Mstahiki meya wa Manispaa ya Moshi Zuberi Kidumo alisisitiza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya mshikamano kati ya baraza la madiwani, timu ya wataalamu wa halmashauri, na wananchi.

“Sisi tumejifunza kuwa maendeleo hayana chama. Mkurugenzi wetu amesimamia vyema ukusanyaji wa mapato na utekelezaji wa miradi, na leo tuna bajeti inayotekelezeka kwa zaidi ya asilimia 60, kitu ambacho hakijawahi kutokea katika miaka ya nyuma,” alisema Mwenyekiti huyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Moshi Mwajuma Nasombe akitokwa na machozi amewashukuru viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Moshi kwa kutambua mchango ambao watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi wafanya kwa niaba ya wananchi .

Hatua hii ya mshikamano wa kisiasa imeibua mjadala mpana kuhusu umuhimu wa kushirikiana kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, huku wadau wa siasa wakisema kuwa inaweza kuwa mfano kwa halmashauri nyingine nchini.

Related Posts