Mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU), Mahmoud Youssouf wa Djibouti ameshinda nafasi hiyo.
Mahmoud Youssouf ameshinda nafasi hiyo kwa kupata kura 33. Wagombea wengine walikuwa Raila Odinga wa Kenya na Richard Randriamandrato kutoka Madagascar.
Odinga alikuwa akiwania nafasi hiyo na wagombea wengine ili kumpata atakayemrithi Moussa Faki Mohamed, Waziri Mkuu wa zamani wa Chad anayetarajia kumaliza muhula wake wa pili wa uenyekiti wa AU mapema mwakani.
Hii ni mara ya pili Kenya kutupa karata yake katika kuwania nafasi hiyo, ilifanya hivyo mwaka 2017 alipogombea Amina Mohammed lakini hakufanikiwa.
Katika uchaguzi wa nafasi hiyo, wakuu wa nchi za Afrika, wamepiga kura kwa siri na inahitaji kupata angalau theluthi mbili ya 36 ili kumpata mshindi.
Endelea kufuatilia Mwananchi