Aziz KI, Hamisa imeisha hiyo

KIUNGO wa Yanga, Stephanie Azizi Ki na mwanamitindo, Hamisa Mobetto hatimaye wamemaliza utata baada ya mchana wa leo kufunga ndoa na kuanza maisha rasmi ya mke na mume.

Wawili hao waliibua utata baada ya kuzagaa kwa matangazo ya kuwepo kwa ndoa hiyo, kiasi kuna baadhi ya mashabiki hawakuamini kama kuna kitu kama hicho kabla ya jana usiku Hamisa kutolewa mahari kisha kufishwa pete ya uchumba na leo mchana kwenye Msikiti Nuur, uliopo Mbweni jijini Dar es Salaam wawili hao kufungishwa ndoa.

Ndoa hiyo ya mastaa hao, ilifungishwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam, Sheikh Walid Alhad Omar na kusikindikizwa na maulidi, huku kukiwa na furaha, shangwe, nderemo na vifijo kwa maharusi, wanafamilia na mashabiki wa wawili hao kuthibitisha kuwa kwa sasa wao ni mke na mume.

Katika shughuli hiyo ya kihistoria kwa wawili hao, Azizi Ki ameandamana na viongozi  wa Yanga wakiongozwa na Rais wa klabu, Injinia Hersi Said, ambaye ndiye amesimamia mipango yote ya harusi hiyo kwa niaba ya wazazi wa Azizi Ki na watu wake wa karibu wengine .

Ilikuwa ni baada kusomwa kwa Qur’an ndipo Sheikh Walid  akakinyanyua kiganja cha Azizi Ki na kumuozesha kwa Hamisa Mobetto.

“Mimi Stephane Azizi Ki nimekubali kumuoa Hamisa Mobetto kwa mahari tuliyokubaliana na ikitokea sababu ya kuachana tuachane kwa wema,” amenukuliwa Aziz Ki wakati akifunga ndoa hiyo.

Katika shughuli hiyo, Azizi Ki  alivaa joho na kilemba, alishika upanga kama desturi ya tamaduni ya zinavyomtaka na baada ya kutoka msikitini waalikwa wamekwenda nyumbani kwa ndugu wa Hamisa Mobetto nyumbani kwao Bahari Beach jijini Dar es Salaam.

Ktika msafara wa maharusi hao, zaidi ya magari 10 ya kifahari yaliwabeba wahusika na sasa wawili hao wanajiandaa kwa sherehe ya kukata na shoka iliyopangwa kufanyika Jumatano ya Februari 17, jijini Dar es Salaam.

Related Posts