Mwanamitindo, muigizaji na msanii wa muziki wa Kizazi Kipya nchini Tanzania, Hamisa Mobetto leo, Februari 16, 2025 amefunga ndoa na mchumba wake, nyota wa klabu ya Yanga SC na raia wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki.
Tukio hilo la kihistoria limefanyika Msikiti wa Mbweni , jijini Dar es Salam na likihudhuriwa na watu maarufu kibao.