Shakira Ashindwa Kufanya Shoo, Akimbizwa Hospitali – Global Publishers



Staa wa Pop duniani, Shakira

Staa wa Pop duniani, Shakira, amelazimika kukatisha shoo yake nchini Peru na kukimbizwa hospitali baada ya kupatwa na maradhi ya tumbo.

Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii, Shakira amewaomba radhi mashabiki wake kwa kushindwa kupafomu.

“Nasikitika kuwataarifu kuwa jana usiku nilipata dharura ya kiafya, nilikimbizwa hospitali baada ya kuugua tumbo, bado naendelea na matibabu,” aliandika.

Katika taarifa yake, Shakira alisema anatarajia kupona hivi karibuni. “Mpango wangu ni kufanya shoo hii haraka iwezekanavyo. Timu yangu na waandaaji tayari wanafanya kazi ya kupanga tarehe mpya,” alisema.

Mwanamuziki huyo kutoka Colombia aliwasili Lima, mji mkuu wa Peru, Jumamosi, ikiwa ni mara yake ya kwanza kwa takribani miaka 10 kufanya shoo nchini humo.

Shakira yupo kwenye ziara ya kimuziki akiutangaza albamu yake mpya Las Mujeres Ya No Lloran, ambapo anahusisha safari yake ya talaka iliyopewa uangalizi mkubwa wa vyombo vya habari katika muziki wake. Albamu hiyo inajumuisha kibao maarufu duniani Shakira: Bzrp Music Sessions, Vol. 53, ambacho kilishinda tuzo ya “Best Latin Pop Album” katika Tuzo za Grammy 2024 mapema mwezi huu.

Ziara yake inaendelea katika mataifa mbalimbali ya Amerika ya Kusini kabla ya kuelekea Canada na Marekani mwezi Mei kwa mfululizo wa maonyesho yatakayoendelea hadi Juni.


Related Posts