Na.
Mwandishi Jeshi la Polisi- Arusha
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Arusha limesema kwa kipindi cha kuanzia mwezi Januari, 2025
hadi Februari 2025 lilifanya operesheni dhidi ya uhalifu na wahalifu na
kufanikiwa kukamata watuhumiwa mbalimbali
na kuwafikishwa Mahakamani.
Akitoa
taarifa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamjzi wa
Polisi SACP Justine Masejo amesema kuwa kwa upande wa makosa ya ukatili na
unyanyasaji wa kijinsia, walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa 15 na kuwafikisha mahakamani, ambapo
kati yao 10 walikamatwa kwa tuhuma
za ubakaji na wengine 05 kwa tuhuma
za ulawiti
Ameongeza
kuwa baada ya kufikishwa Mahakamani kwa tuhuma za ubakaji, Watuhumiwa 03 walihukumiwa vifungo vya maisha
Jela, 01 kifungo cha miaka 30. Aidha mtuhumiwa 01 amehukumiwa kifungo cha maisha jela
na mwingine 01 kifungo cha miaka 30 kwa tuhuma za ulawiti. Watuhumiwa
wengine kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.
SACP
Masejo amebainisha kuwa Kupitia misako dhidi ya dawa za kulevya walifanikiwa
kukamata Watuhumiwa 26 wakiwa na
Mirungi Kilogramu 196.4, Watuhumiwa 22 wakiwa na Bhangi kilogramu 32 pamoja na kuteketeza zaidi
ya hekari 10 za bhangi.
Aidha
amefafanua kuwa watuhumiwa wote wa Dawa za kulevya tayari wamefikishwa
Mahakamani na kesi zao zipo katika hatua mbalimbali.
Vilevile
kamanda Masejo ameeleza kuwa Kwa upande wa mapambano dhidi ya ujangili, walifanikiwa
kukamata watuhumiwa 02 wakiwa na
nyama ya Nungunungu kilogramu 20 ambapo tayari wamefikishwa Mahakamani na kesi
zao zipo katika hatua mbalimbali.
Sambamba
na hayo amesema kuwa kwa kipindi hicho walifanikiwa kukamata Watuhumiwa 38 wakiwa na pombe ya Moshi lita 172 na mitambo 04 ya kutengenezea pombe hiyo ambapo watuhumiwa wote tayari
wameshafikishwa Mahakamani kwa taratibu za kisheria huku watumiwa 202 wa makosa
ya wizi wakikamatwa katika operesheni hiyo.
Jeshi
la Polisi Mkoa wa Arusha likatoa rahi kwa kwa baadhi ya watu wachache
wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kuacha mara moja vitendo hivyo kwani
tutawakamata na kuchukua hatua za kisheria dhidi yao Pamoja na madereva
wanaoendesha vyombo vya moto kufuata sheria za usalama barabarani.