Mikoa 15 kupata mvua kuanzia saa 3 usiku huu

Dar es Salaam. Baadhi ya maeneo ya mikoa 15 inatarajiwa kupata mvua kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku, kwa mujibu wa Mamlala ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Mikoa hiyo ni pamoja na Kagera, Geita, Kigoma, Tabora, Katavi, Morogoro, Rukwa, Ruvuma, Iringa, Songwe, Njombe, Lindi, Mtwara, Rukwa na Mbeya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumanne Februari 18, 2025 na TMA imeeleza kuwa baadhi ya maeneo machache ya mikoa hiyo yatakuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo sambamba na vipindi vya jua.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa visiwa vya Unguja na Pemba, mikoa ya Singida, Dodoma, Dar es Salaam, Tanga, Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mwanza, Simiyu, Pwani ikujumuisha visiwa vya Mafia kutakuwa na mawingu kiasi na vipindi vya jua.

“Upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa katika Pwani yote. Kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini, wakati hali ya bahari inatarajiwa kuwa mawimbi makubwa kiasi,” imeeleza taarifa hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts