WIZARA Ya Elimu,Sayansi na Teknolojia itaendelea Kushirikiana na Wadau Mbalimbali wa Elimu hususani Taasisi na Mashirika Kuhakikisha Mazingira rafiki Kwa Kujifunzia na Ufaulu Unaongezeka Mashuleni.
Akizungumza na Wanahabari wakati wa akizindua Mradi wa Elimu wa Mafunzo kwa Walimu wa Shule za Awali ( CORE) kupitia Shirika la Montessori Mwakilishi Kutoka Wizara ya Elimu ambae ni Mratibu Idara ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Dkt. Hawa Juma Seleman amesema Hatua hiyo ya Mradi huo ni Utekelezaji wa Elimu Kwenda Kwenye ubora ili Kumuendeleza mtoto wa shule za awali Kuweza Kujifunza akiwa ngazi ya chini.
Aidha Seleman ameendelea zaidi na Kusema Kuwa Wizara ya Sayansi na Teknolojia Wamesaini Hati ya Makubaliano na Shirika la Montessori pamoja na Ofisi ya Rais Tamisemi ili waweze Kufanya kazi pamoja Kumuendeleza mtoto wa shule za awali.
“Tumesaini Hati ya Makubaliano na Tumekubaliana Katika Maeneo Matano ikiwemo eneo la Kumuendeleza mtoto katika ujifunzaji wa awali na ujumuishi ,eneo la ushirikishwaji wa jamii na uwekezaji kwa Watoto,uendelezaji maswala ya watoto kwa kushirikisha Viongozi ikiwemo Walimu wa elimu ya Awali pamoja na Kumuendeleza Mwalimu Kitaaluma”.
Seleman ameongeza kuwa Shirika lolote linapojitokeza kuweka nguvu na kushirikiana na Serikali linalenga Kusaidia Serikali pale inapotakikana ili kufikia malengo hivyo tupo Pamoja kuhakikisha watoto wanapata hayo mahitaji ya jumla.
Pia ametoa wito kwa taasisi na Mashirika mengine kujitokeza kuunga Mkono Serikali Kuhakikisha Watoto wa Awali Wanapata Mahitaji ya jumla,Wanajifunza ,Wanakuwa na Mahitaji yao kwa ujumla.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Montessori Sara Kiteleja amesema Mradi huo ni hatua Muhimu katika Kuimarisha Elimu ya awali nchini kwa Kuhakikisha Kwamba Watoto wanapata msingi bora wa Kujifunza kupitia mbinu za Montessori zinazojikita katika mazingira ya jamii husika.
Kiteleja amefafanua zaidi Kuwa Mradi huo umeanzishwa Kwa nia ya Kuhakikisha Kwamba Walimu wa Elimu ya awali wanaendelea Kupata mafunzo Kazini ,yatakayowasaidia kuimarisha na kuboresha Mazingira ya kufundishia na Kujifunza kwa Kuzingatia sera ya Elimu na Mafunzo 2014 toleo la Mwaka 2023.
Hata hivyo amesema Mradi huu utatekelezwa kwa awamu mbalimbali ambapo awamu ya kwanza itakuwa ya Majaribio (Pilot phase) mwaka huu 2025.
Pia ameongeza kuwa mradi huo utafanyika katika Mikoa ya Singida ,Unguja na Zanzibar yatachochea upanuzi wa mradi katika maeneo mengine yenye uhitaji zaidi ndani ya Tanzania .
“Katika mradio huo Mkoa wa Singida takribani Walimu 127 Zanzibar Walimu 80 hivyo Jumla ya Walimu 207 Watanufaika na mradi huo.”
Mkurugenzi wa Shirika la Montessori Sara Kiteleja akizungumza na Wanahabari na Wadau Wa Elimu Mara baada ya Kuzinduliwa Kwa Mradi wa Elimu wa Shirika la Montessori ( CORE) ambao Mafunzo yatawafikia Walimu wa Shule za awali Kwa Mkoa wa Unguja, Singida na Dar es Salaam .
Mratibu wa Idara ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Dkt. Hawa Seleman akizungumza Wakati wa Uzinduzi wa Mradi wa Mafunzo Kwa Walimu wa Shule za Awali (CORE) uliofanyika Msimbazi Center Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Idara ya Elimu, Maandalizi na Msingi Fatma Ramadhan akitoa pongezi Kwa Shirika la Montessori Kuiunga Mkono Serikali katika nyanja ya Kuboresha Mazingira ya Kujifunza Kwa Walimu wa Shule za Awali na Kuhakikisha Walimu Kutoka Visiwani Zanzibar Watanufaika na Mradi huo