WALIMU SHINYANGA WAGUSWA NA KLINIKI YA SAMIA

Walimu wa Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika Kliniki ya Samia ya kutatua changamoto za walimu.
*RC Macha asema Kliniki ya Samia kutibu chnagamoto za walimu
*Makamu wa Rais CWT asema watashughulika na watumishi wasioshughukia changamoto walimu.
Na Mwandishi Wetu,Shinyanga
MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Annamlingi Macha amesema kuwa Kliniki ya Samia kwa imekuja wakati mwafaka katika kutatua changamoto za Walimu kutokana na kushirikisha taasisi zinazohusika moja kwa moja na walimu.
Macha ameyesema hayo wakati akufungua Kliniki ya Samia kwa Walimu wa Mkoa Shinyanga ,amesema kuwa Kliniki hiyo inatoa fursa kwa changamoto zao kutatuliwa na kufanya walimu kuwa na utulivu.
Amesema kuwa changamoto hizo zinakwenda kuisha kutokana na kuwepo kwa Taasisi kushughulika na walimu moja kwa moja na kama kuna changamoto kwenye madai hayo itakuwa na maelekezo tu ya kufanya utatuzi.
Aidha amesema kuwa kuwa walimu wana fursa ya kuongeza kipato chao kwa kufanya shughuli za kuongeza kipato ambazo hazitaathiri ufundishaji wao.
Amesema kuwa walimu hawana sababu ya kuingia mikopo ya kuwaumiza wakati taasisi za fedha zipo na zinatoa riba ndogo ambapo kazi ya mwalimu kutengeneza biashara ya kufanyia mkopo anaopata.
Makamu wa Rais wa Chama Walimu Tanzania (CWT)Mwalimu Seleman Ikomba amesema kuwa Kliniki ya Samia wanairatibu katika kutatua changamoto za walimu.
Amesema kuwa maafisa watumishi wanaokwamisha madai ya walimu watashughulika nao moja kwa moja ili kuhakikisha walimu wanalipwa stahiki zao.
Ikomba amesema tangu kuanza kwa Kliniki ya Samia imekuwa na matokeo makubwa kutokana na walimu kuhudumiwa na dawati lenye maafisa taasisi tano ambazo zinazunguka katika Kliniki hiyo.
Mwalimu Policapy Muchunguzi amesema kuwa huduma ya Kliniki ya Samia ni nzuri kutokana na kupata huduma moja kwa moja kwa taasisi zinazohusika na walimu.
Amesema kuwa walimu ambao hawajafikiwa na Kliniki wajiandae wakifiwa wawe na vielelezo vya madai.

Related Posts