Watano wafa maji, wamo watatu wa familia moja

Watu watano wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia baada ya kuzama kwenye la maji lililopo jirani na makazi yao katika Kijiji cha Bulige, Halmashauri ya Msalala, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Akithibitisha tukio hilo leo Jumanne Februari 18, 2025, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wilayani Kahama, Stanley Luhwago amewataja waliofariki dunia ni Zawadi Nkwambi (13), Khadija Nkwambi (11), Rahel Peter (11), Samike Peter (1) pamoja na mama mzazi wa Samike, Hoja Kubo (29) aliyefariki wakati akijaribu kuwaokoa wanaye wawili.

Mama aliyepoteza watoto wake wawili katika tukio hilo, Prisca Luchagula amesema lilitokea Februari 15, 2025 saa 10 jioni, watoto wawili kati yao walipoanza kuogelea baada ya kutoka shambani.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Mboni Mhita akitoa pole kwa familia zilizofikwa na watu watano wakiwemo watatu wa familia moja waliozama kwenye dimbwi la maji katika shimo lililokuwa likitumiwa kuchimba madini ya ujenzi kijiji na kata ya Bulige, Halmashauri ya Msalala. Picha na Amina Mwambo

Amesema wakati wakiendelea kuogelea, maji yaliwazidi nguvu na kuzama hali iliyosababisha mama aliyekuwa jirani kutumbukia wakati akiwa katika jitihada za kuwaokoa watoto hao ndipo naye akazama na watoto wake wawili waliokuwa pembeni nao wakaingia kutaka kumwokoa mama yao nao pia wakazama na kufariki.

Endelea kufuatilia Mwananchi.

Related Posts