Dar es Salaam. Mwalimu wa Madrasa, Musa Bashiru Musa (24) ambaye kipande cha picha jongefu (video) kilisambaa katika mitandao ya kijamii kikimuonyesha akiwapiga fimbo za mikononi wanafunzi wake, amepandishwa kizimbani kujibu tuhuma zake.
Musa ambaye ni mkazi wa Mbagala Kiburugwa, amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke na kusomewa mashtaka mawili ya kuwafanyia ukatili watoto wa madrasa, kinyume cha sheria.
Mwalimu huyo amefikishwa mahakamni hapo leo Jumatano, Februari 19, 2025 na kusomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Rabia Ramadhani akisaidiana na Nicas Kihemba, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Vick Mwaikambo.
Endelea kufuatilia Mwananchi.