KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA, KATIBA NA SHERIA YAIPONGEZA TEA KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA ELIMU ZANZIBAR

– Kamati yaridhishwa na utekelezaji wa miradi ya elimu Zanzibar
-Miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.8 imetekelezwa
-Vijana 600 kutoka kaya maskini wamenufaika na Mafunzo ya Ujuzi

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imeipongeza Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa utekelezaji mzuri wa majukumu yake, hususani miradi ya elimu inayotekelezwa Zanzibar. Pongezi hizo zimetolewa kutokana na juhudi kubwa zinazofanywa na TEA katika kuboresha miundombinu ya elimu na kuongeza fursa za ujifunzaji na ufundishaji katika ngazi zote za elimu.

Awali katika taarifa iliyowasilishwa mbele ya Kamati leo Februari 19, 2025 na Mkurugenzi Mkuu wa TEA, Dkt. Erasmus Kipesha ilibainisha kuwa, ndani ya kipindi cha miaka mitano (2019/2020 – 2024/2025), TEA imetekeleza miradi mbalimbali yenye thamani ya takribani Shilingi Bilioni 2.8. Kati ya kiasi hicho, Shilingi Bilioni 2.1 zimetumika kuboresha miundombinu ya elimu, huku Shilingi Milioni 574.3 zikielekezwa katika kufadhili Mafunzo ya Kuendeleza Ujuzi (SDF) kwa vijana 600 kutoka kaya maskini.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria Mhe. Florent Kyombo alitoa pongezi hizo kwa niaba ya Kamati wakati wa ziara ya kikazi kisiwani Unguja Zanzibar, Februari 19, 2025. Ziara hiyo ililenga kukagua na kutathmini maendeleo ya miradi ya elimu inayotekelezwa na TEA pamoja na kupokea taarifa ya utekelezaji wa shughuli za muungano katika sekta ya elimu.

Mhe. Kyombo alisisitiza kuwa TEA imefanya kazi kubwa katika kuboresha miundombinu ya elimu, na miradi yake imekuwa na manufaa makubwa kwa jamii. Alibainisha kuwa hata jimboni kwake, TEA imetekeleza miradi kadhaa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa, hali inayoonyesha mchango mkubwa wa TEA katika kuinua ubora wa elimu nchini.

“Mamlaka ya Elimu Tanzania inafanya kazi kubwa sana kwenye uboreshaji wa miundombinu ya elimu kote nchini, siyo Zanzibar pekee. Ukipita maeneo ya vijijini na pembezoni mwa miji, utaiona miradi yao mingi ambayo inaendelea kutatua changamoto za miundombinu ya elimu,” alisema Mhe. Kyombo.

Aidha, Kamati iliishauri TEA kupanua wigo wa utekelezaji wa miradi ya uendelezaji ujuzi ili kutoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi kunufaika, hasa katika kuwajengea vijana uwezo wa kujiajiri na kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Dkt. Leonard Akwilapo, aliishukuru Kamati ya Bunge kwa kutambua juhudi za Mamlaka hiyo na kuahidi kuendelea kusimamia kwa weledi utekelezaji wa miradi yote ya elimu Tanzania Bara na Zanzibar. Pia alisisitiza kuwa TEA itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutafuta rasilimali kifedha ili kufadhili miradi mingi zaidi kwa maendeleo ya sekta ya elimu hapa nchini.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo (kulia), pamoja na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira, Mhe. Khamis Chilo, wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa majukumu na miradi ya elimu upande wa Zanzibar kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Dkt. Erasmus Kipesha (hayupo pichani).

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakisikiliza na kufuatilia taarifa ya utekelezaji wa majukumu na miradi ya elimu upande wa Zanzibar iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Dkt. Erasmus Kipesha.

Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Dkt. Leonard Akwilapo (kushoto), akifuatilia taarifa ya utekelezaji wa majukumu na miradi ya elimu upande wa Zanzibar iliyowasilishwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Dkt. Erasmus Kipesha, mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakisikiliza na kufuatilia taarifa ya utekelezaji wa majukumu na miradi ya elimu upande wa Zanzibar kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Dkt. Erasmus Kipesha.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania, Dkt. Erasmus Kipesha, akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu na miradi ya elimu upande wa Zanzibar mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

Mwenyekiti wa Bodi ya TEA, Dkt. Leonard Akwilapo (kushoto), akifafanua jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria mara baada ya kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa majukumu na miradi ya elimu upande wa Zanzibar.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Mhe. Florent Kyombo (wa pili), akiongoza msafara wa wajumbe wa kamati kukagua ujenzi wa jengo la maabara mbili zilizofadhiliwa na TEA katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST).

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, Bw. Khamis Said, akiwaonesha kitu baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria walipokuwa katika ziara ya kukagua miradi iliyofadhiliwa na TEA katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST).

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakikagua ujenzi wa jengo la maabara mbili zilizofadhiliwa na TEA katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST).

Baadhi ya watumishi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania wakiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria wakati wa ukaguzi wa ujenzi wa jengo la maabara mbili zilizofadhiliwa na TEA katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Karume (KIST).

Related Posts