Kisarawe. Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Tanganyika Masele, mkulima ambaye ni mkazi wa Kiisangile, Kata ya Marui, Wilaya ya Kisarawe mkoani humo kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya mkewe na mtoto wake mchanga.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani, Salim Morcase aliyoitoa jana Jumanne Februari 18, 2025 ilisema tukio hilo lilitokea Jumatatu saa 7 mchana, Kitongoji cha Buduge Kata ya Marui Wilaya ya Kisarawe.
Kamanda Morcase amewataja waliouawa ni Gumba Kulwa ambaye ni mke wa mtuhumiwa na mtoto wao, Masele Tanganyika.
“Miili ya marehemu hao imekutwa nyuma ya nyumba yao jirani bwawa la maji na mtoto huyo ambaye ni marehemu kwa ana miaka miwili na miezi minne,” imeeleza taarifa hiyo.
Amesema marehemu hao waliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni ikielezwa kuwa chanzo ni wivu wa mapenzi na kwamba awali mtuhumiwa huyo alikuwa akitoa vitisho kwa mkewe kuwa atamdhuru.
Amesema baada ya polisi kupata taarifa hiyo ilianza uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vingine na hatimaye kumkamata mtuhumiwa huyo.
Amesema wanaendelea kumshikilia mtuhumiwa kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi utakapokamilika watamfikisha mahakamani huku miili ya miili ya marehemu ikihifadhiwa katika Hospitali ya Kisarawe