NJIRO; WANANCHI SIO LAZIMA KUFANYA WIRING NYUMBA NZIMA MNAWEZA KUFANYA CHUMBA KIMOJA KWAAJILI YAKUPOKELEA UMEME

 NA BELINDA JOSEPH, SONGEA

Wakazi wa Kata ya Subira Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma, wametakiwa kuunganisha nyaya za umeme angalau chumba kimoja kwenye Nyumba ili kuwawezesha kupata huduma hiyo mapema badala ya kusubiri REA watakapoukabidhi mradi huo kwa TANESCO jambo ambalo litasababisha gharama yakuunganisha umeme kupanda kutoka Ile ya mradi wa REA shilingi elfu 27.

Akiwa katika mwendelezo wa  ziara yake ya utoaji elimu kwa wananchi waliofikiwa na miradi mipya ya umeme Manispaa ya Songea hii leo, Afisa Uhusiano na huduma kwa Wateja kutoka Shirika la umeme Tanzania TANESCO  Mkoa wa Ruvuma Alan Njiro, amewataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo mapema Kadri inavyowezekana ili kuwawezesha kuupokea umeme huo na baadae wataendelea kuunganisha katika vyumba vingine kwenye nyumba zao.

Amesema Ndani ya Mwezi mmoja Wakazi wa maeneo ya Kisiwani C na maeneo jirani yaliyopitiwa na miradi  kwenye Kata hiyo, watakuwa wamefungiwa nyaya kwenye nguzo ambazo tayari zimekwisha simikwa hivyo waendelee kufanya wiring ili umeme utakapowashwa wapate huduma hiyo moja kwa moja.

Amewataka  kuwa makini hususani katika kipindi hiki ambacho watakuwa wanataka kufanyiwa uunganishaji wa nyaya za umeme n.k hivyo wawe makini kutoa taarifa TANESCO kwani zoezi zima la maombi ya umeme linafanyika kwa njia  ya App ya NIKONEKTI, simu janja, simu ya kitochi au kufika katika ofisi zao kwa ufafanuzi zaidi nasio kumpa pesa mtu atakaejitambulisha kama mtumishi wa shirika hilo.

Akiendelea na utoaji wa elimu Njiro, ameeleza kuwa wananchi pindi wanapotaka kukata miti ni lazima wawasiliane na TANESCO wazime laini hiyo ya umeme ili kusaidia kuepuka changamoto kwa wananchi pindi watakapokata vibaya na kuigusa miundombinu hiyo ambayo ni hatari inayoweza kuleta athari kwa jamii ikiwemo vifo.

Wakizungumza wananchi wa Kata hiyo Mara baada ya kupokea elimu kutoka TANESCO, wameonyesha kuridhishwa na elimu hiyo huku wakiahidi kuendelea kushirikiana na Shirika ili kuepuka matapeli ambao wanaweza jitokeza katika hatua za kuunganishiwa Nyaya za umeme hivyo itawalazimu kuwasiliana na kufika TANESCO pindi watakapohisi uwepo wa dalili za utapeli.

Diwani wa Kata ya Subira John Ngonyani, ameishukuru TANESCO kuhakikisha mitaa yote nane inafikiwa na miundombinu ya umeme huku akiwataka kuendelea na ushirikianao huo huo ili kuwafikia wananchi wote, akiipongeza Serikali Mbunge Damas Ndumbaro, pamoja na Meneja wa TANESCO kushirikiana kwa pamoja katika maendeleo.

Related Posts