Mohamed Baresi aanza mikwara Ligi Kuu

MASHUJAA juzi jioni ilikuwa uwanjani mjini Kigoma na kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Pamba Jiji, huku kocha wa timu hiyo Mohamed Abdallah ‘Baresi’, akianza mikwara wakati akijiandaa kuikabili Yanga keshokutwa Jumapili mjini humo.

Mashujaa ilikuwa imecheza mechi nane mfululizo bila kuonja ushindi kwani mara ya mwisho iliifunga Namungo kwa bao 1-0  Novemba 23 mwaka jana kabla ya juzi kuzinduka na matokeo hayo yamempa nguvu kocha Baresi wakati wakijiandaa kuipokea Yanga Jumapili hii.

Yanga inatarajiwa kuondoka leo kwenda Kigoma kuwahi pambano hilo, lakini wenyeji wakitamba ushindi wa juzi umewapa nguvu ya kuwakabili vinara hao wa Ligi Kuu wakiwa na pointi 52 baada ya mechi 20 kwa nia ya kuhakikisha inajiweka mahali pazuri.

Baresi ameliambia Mwanaspoti anajua ana kazi kubwa ya kufanya kuikabili Yanga ambayo ipo kileleni kwa ubora na wao wanapambana kutafuta matokeo mazuri, kwani wamepoteza pointi nyingi katika mechi nane walizocheza bila ushindi kwa kutoka sare nne na kupoteza nne.

Kupoteza mechi nne ina maana Mashujaa iliangusha pointi 12 na sare nne ni pointi nane na katika mechi hizo nane imepoteza pointi 20, kitu ambacho kimewaacha nyuma kulinganisha na matarajio waliyokuwa nayo awali.

Mashujaa wataikabili Yanga ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa mabao 3-2, lakini tangu ipande Ligi Kuu msimu uliopita haijawahi kutamba mbele ya watetezi hao wa ligi kwa vile ilipoteza mechi zote zilizopita kwa kufunga 1-0 na 2-1 mtawalia.

Baresi alisema anajua soka ni mchezo wa makosa, hivyo unapokosea kidogo ni lazima uadhibiwe na kwa ubora wa Yanga hawataki kufanya kosa litakalowaumiza zaidi wakiwa nyumbani.

“Hautakuwa mchezo rahisi tutaingia kwa kuwaheshimu wapinzani wetu, lakini huo mchezo kwetu ni muhimu sana tunazihitaji pointi tatu muhimu tukiwa kwenye uwanja wa nyumbani,” alisema Baresi aliyeiwezesha timu hiyo kufikisha pointin 23 katika mechi 20 na kushika nafasi ya sita kwa sasa.

v Fountain Gate (nyumbani)

v Tabora United (nyumbani)

v JKT Tanzania (nyumbani)

Related Posts