COY ATUNUKIWA TUZO YA HESHIMA (TCA)

Mwanzilishi wa Jukwaa la Ucheshi (Cheka tu) Conrad Kennedy Coy amepewa Tuzo ya Heshima Katika Usiku wa Tuzo za Ucheshi (TCA) unaofanyika Ukumbi wa Superdom Masaki Jijini Dar es Salaam.

Coy amekuwa akitoa Mchango wake Mkubwa na Kufanya Mapinduzi ya burudani ya Ucheshi Kipindi cha hivi Karibuni .

Aidha Coy amekuwa akilea Wasanii wa Ucheshi na Kuwaandalia Majukwaa mbalimbali ili Kuendelea Kuonesha na Kukuza Vipaji vyao ,
Miongoni mwa Waliopita katika Mikono yake ni pamoja na Asma Jameda,Mama chanja,Kipotoshi na Wengine wengi.

Mara baada ya Kupokea tuzo hiyo Coy amemtaja Mpoki,Marehemu Max na Zembwela Kama Walimu ambao wamempa njia ya Kufika hapo alipo.

Related Posts