Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Ndugu Jokate Urban Mwegelo (MNEC) ameongoza Maelfu ya Vijana Korogwe katika Matembezi ya Amani ya maandalizi ya Mapokezi ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anayetarajia kuanza Ziara yake ya kikazi Mkoani Tanga tarehe 23 Februari, 2025.
Katika Matembezi hayo, Ndugu Jokate aliongozana na Ndg. Thobias Nungu, Mwenyekiti wa CCM Korogwe mjini, Ndg. Jessica Mshama, Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UVCCM Taifa, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Korogwe Mjini, pamoja na Viongozi wengine wa Chama na Serikali.