RISING STAR FC NA KAMILI GADO FC ZAPEWA JEZI

KAMA kawaida leo hii ni siku nyingine tena ambapo wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet walifunga safari hadi Kawe kwaajili ya kutoa vifaa vya michezo kama jezi kuzisapoti timu za Rsing Star na Kamili Gado.
Kampuni hiyo imetoa msaada wa vifaa vya michezo kwa timu ya Rising Star FC na timu ya Kamili Gado. Msaada huu ni sehemu ya mchango wa Meridianbet katika kuunga mkono maendeleo ya soka na kukuza vipaji vya vijana nchini.
Timu ya Rising Star FC, inayoshiriki katika ligi mbalimbali za ndani, imepata jezi hizo za kisasa kwaajili ya mazoezi na mashindano, huku pia wakishinikiza umuhimu wa kuwekeza katika vijana jinsi ambavyo Dunia inaenda. Hii itawawezesha wachezaji wa timu hiyo kufanya mazoezi kwa ubora na kuongeza uwezo wao katika uwanja wa michezo.
Kwa upande wa michezo Jumamosi ya leo, suka jamvi lako na Meridianbet huku ukikumbuka kucheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.
Aidha, timu ya Kamili Gado, baada ya kupokea msaada huo wa jezi walisema kuwa wanaishukuru sana Meridianbet kwa kuwaletea jezi hizo na kutambua umuhimu wao kwenye sekta ya michezo kwani walikuwa na uhitaji mkubwa wa jezi hizo ambazo zinaweza kuwasaidia kwenye mashindano yao mbalimbali ambayo hushiriki.
Lakini pia wanawaomba Meridianbet wazidi kufika kwenye timu mbalimbali za mpira ambazo ni changa kwani timu hizi huwa zinahitaji sana kushikwa mkono ili kuweza kuendeleza vipaji vyao na ndoto zao za kila siku.
Katika zoezi la ugawaji wa jezi hizo, Mwakilishii wa Meridianbet Bi Nancy Ingram alisema: “Tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya Rising Star FC na Kamili Gado. Tunatambua umuhimu wa kuwapa wachezaji vijana na wale walioko kwenye hatua za juu vifaa bora ili waweze kufikia malengo yao. Meridianbet itazidi kushirikiana na wadau wa michezo ili kuchangia katika ukuaji wa michezo nchini.”
Aidha Meridianbet wameendeleza jitihada zao za kuendeleza kukuza michezo nchini, hasa kwa kuzingatia umuhimu wa kusaidia timu na wachezaji kwa vifaa na rasilimali zitakazowawezesha kufikia viwango vya juu zaidi katika ufanisi wa michezo. Jisajili na ubeti na Meridianbet.

Related Posts