Gomez aanza na sare Wydad, bao alilotupia lakataliwa

MSHAMBULIAJI wa Kitanzania anayekipig Wydad AC ya Morocco, Seleman Mwalimu ‘Gomez’ ameanza mechi ya kwanza akiwa na uzi wa timu hiyo iliyotoka suluhu na COD Meknes katika mechi ya Ligi Kuu nchini humo maarufu Batola Pro.

Gomez alitambulishwa na vigogo hao wa Afrika,  Januari 31 mwaka huu akitokea Fountain Gate aliyokuwa akiitumiki kwa mkopo kutoka Singida Black Stars.

Mshambuliaji huyo, aliyeondoka katika Ligi Kuu Bara akiwa na mabao sita, ni Mtanzania pekee anayekipiga Botola Pro kwa sasa baada ya nyota kadhaa kupita akiwemo Simon Msuva na Nickson KIbabage waliwahi kuzitumia timu za Difaa El Jadida na Wydad kabla ya kila mmoja kutimka kivyake.

Katika mchezo huo wa juzi jioni, Wydad ilikuwa uwanja wa nyumbani kwa mchezo wa raundi ya 22 ya ligi hiyo na kulazimishwa suluhu hiyo na COD Meknes, huku Gomez akianzia benchi kabla ya kuingizwa dk ya 60 kumpokea Mickael Malsa aliyesaliwa hivi karibuni kutoka Valladolid ya Hispania.

Licha ya straika huyo wa zamani wa KVZ kutumika kwa dakika 30 alionyesha kiwango bora akijaribu kuendana na kasi na presha ya mchezo huo uliojaa mashabiki wengi.

Robo saa baada ya kuwa uwanjani, Gomez alitupia mpira kambani akimalizia shuti la beki Zakaria Nassik, lakini hata hivyo, bao hilo lilikataliwa na mwamuzi aliyetafsiri alikuwa ameotea kabla ya kufunga.

Mwal

Baada ya mchezo huo, akizungumza na waandishi wa habari, kocha wa timu hiyo, Rulani Mokwena alisema; “Tunapoteza pointi nyingi sababu ya makosa ya refa, inakuwa hasara kwa kweli, muda mwingine kama kocha najisikia vibaya, nimeona pasi ya Zakaria na nashangaa kwanini bao la Mwalimu limekataliwa nimeangalia hakuwa katika nafasi ya kuotea wakati pasi ile inapigwa,” alisema Mokwena.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Wydad kuwa nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 40 tofauti ya alama 15 na RS Berkane ambaye anaongoza akiwa nazo 55.

Nyota huyo aliyewahi kuzichezea timu mbalimbali ikiwemo FGA Talents inayoshiriki Ligi ya Championship, KVZ ya Zanzibar akiibuka kinara wa mabao akifunga 20 na assisti saba kwenye mechi 27 kati ya 30.

Related Posts