MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI FURSA YA KUONYESHA JUHUDI KATIKA MAENDELEO.

Na.Vero Ignatus,Arusha

Zaidi ya wanawake 300 wamejitokeza kufanya usafi katika Jiji la Arusha ikiwa ni Hamasa kwaajili ya siku ya wanawake Duniani utakayofanyika kitaifa 8Machi 2025 ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan anatazamiwa kuwa mgeni Rasmi

Akizungumza mwenyekiti wa Kamati ya maandallizi ya Hamasa Hindu Bwengo amesema kuwa maadhimisho hayo yatakuwa ya tofauti na ilivyozoweleka awali, kwani shughuli zitaanza tangu Machi 1, 2025,hivyo amewataka wanawake kujitokeza kwa wingi kushiriki kikamilifiu.

Vilevile Bi Hindu amesema maandallizi yanaendeleea vyema, huku akianisha maeneo waligofanya usafi kwani walianza. Maandamano ya Amani kutoka Ofisi ya Mkuu wa mkoa, uwanja wa Shekhe Amri Abeid Soko la Kilombero na kumalizikia uwanja wa Ngarenaro ambapo michezo mbalimbali ya wanawake itakapofanyika huku akiwataka wanawake kujitokeza kwa wingi siku hiyo

Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati ya michezo Diana Moshi amesema kuwa maadhimisho hayo yatakuwa na michezo ya aina mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mchezo wa asili wa mdako,Rede,mechi za mpira wa miguu kati ya timu maarufu za wanawake, Simba Queens, Yanga princess, JKT Queens na Fountain Gate FC, ili kusherehekea ushiriki wa wanawake katika michezo.

“Mdako ni mchezo asilia wa watoto wa wa Afrika Mashariki wa Mchezo huu unashirikisha watoto wawili na kuendelea ambao hutumia vijiwe au changarawe kumi na mbili ambapo Kati yake moja huteuliwa kuwa malkia Mwenye zamu hulichukua na kulirusha juu na kuanza kuchambua yaliyobakia katika duara dogo au shimo akianza na mojamoja, kisha mawilimawili na kuendelea. Mshiriki anayefanikiwa kuchambua mawe yote bila kudondosha malkia huwa mshindi.

“IPO michezo mingi utakayofanyika kabla ya kufikia kilele chenyewe , hivyo Nawaomba wanawake kunitokeza kwa wingi mchezo kama wa rede, Mdako, kuvuta mamba na mingine mingi mama usibweteke njoo kwani maadhimisho yanawaleta wanawake pamoja na kuondoa tofauti zetu. Alisema.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Arusha Sara Mlacky aliwataka wanawake kuhakikisha watoto ambao hawajaadikishwa kwaajili ya kuanza shule wafanye hivyo kwani ni katika kuwapatia haki yao ya msingi ya Kupata Elimu na kuwajengea msingi bora.

Aidha kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Christian Paul Makonda , Mkoa huo utakuwa mwenyeji wa sherehe kubwa za kuadhimisha Siku ya Wanawake ambapo kwa mara ya kwanza, maadhimisho haya yatakuwa ya kipekee, ambapo sherehe zitaanza tangu Machi 1, 2025, na kudumu kwa siku saba, ikiwa ni sehemu ya Wiki ya Mwanamke,Katika kipindi hicho, wizara nane zitatoa huduma muhimu kwa jamii, ikiwa ni pamoja na huduma za afya, kisheria, na elimu ya fedha.

“Hii ni fursa muhimu ya kuonyesha juhudi za wanawake katika maendeleo na kujenga jamii yenye usawa wa kijinsia.ambapo Maadhimisho hayo yatalenga kuhamasisha usawa wa kijinsia na kutambua mchango mkubwa wa wanawake katika nyanja mbalimbali za jamii.” Alisema.


 

Related Posts