Mukombozi afutiwa kadi, refa akaushiwa

BEKI wa Namungo ya Lindi Derrick Mukombozi hatimaye amefutiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyopewa kwenye mchezo dhidi ya Simba.

Mukombozi alipewa kadi hiyo nyekundu iliyozua utata na mwamuzi Japhet Smarti kutoka Katavi, kwenye mchezi dhidi ya Simba baada ya beki huyo kuwa kua kwenye harakati za kumzuia mshambuliaji Lionel Ateba.

Hata hivyo, kadi hiyo ilionekana kuwashtua wengi kutokana na mikanda ya video kuonyesha hakukuwa na tukio lolote linaloweza kusababisha adhabu ya namna hiyo.

Taarifa iliyotolewa na Kamati ya usimamizi wa ligi imetangaza rasmi kwamba kadi hiyo imeondolewa kwa kile ilichosema maelezo yaliyopo kwenye ripoti ya mwamuzi hayakuwa na ushahidi wa kutosha unaoonendana na marejeo ya picha mjongeo.

Wakati kamati hiyo ikiifuta kadi hiyo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwa Smarti aliyetoa maamuzi hayo ya kadi kwa Mulokozi.

Kwa upande mwingine beki wa Namungo Daniel Amoah ametozwa faini ya sh 500000 kwa kosa la kuonekana akimwaga vimiminika kwenye goli jambo linalohusishwa na vitendo vinavyoashiria imani za kishirikina tukio ambalo lilitokea kwenye mchezo huo dhidi ya Simba ambao wekundu hao walishinda kwa mabao 3-0.

Related Posts