NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATEMBELEA ENEO LA UJENZI WA VIWANDA VYA KUBANGUA KOROSHO MKOANI MTWARA

NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Dk. Hussein Mohamed leo tarehe 23 Februari 2025 ameafanya ziara Mkoani Mtwara iliyolenga kutembelea eneo linalotarajiwa kujengwa viwanda vya Kubangua Korosho.

Uwekezaji huo ambao awamu ya kwanza inatarajiwa kugharimu zaidi ya Shilingi Bilioni 300, unatekelezwa kwenye eneo la Maranje Halmashauri ya Mji Nanyamba Wilaya ya Mtwara Mkoani humo.

Amesema serikali pekee hawezi kuendelesha kongoni hiyo, hivyo wanahitaji uwekezaji kutoka sekta binafsi ambao wako tayari kufanya uwekezaji hivyo kutoka katika maeneo mbalimbali Duniani.

‘’Lengo la serikali ifikapo mwaka 2030 ni kuwa asilimia 100 ya korosho inayozalishwa nchini ibanguliwe nchini, maana yake ni lazima tuwe na viwanda vya kutosha vya kubangua nchini na hii siyo Korosho pake yake,hata ufuta pia unatakiwa kukamuliwa hapa nchini, kwahiyo lazima tuwe na hivi viwanda vya kutosha vya kuongeza thamani’’amesema Hussein

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa CBT, Mangile Malegesi amesema eneo lote hilo la kongani lina jumla ya hekari 1,572 na linalotarajiwa kuwa viwanda zaidi ya 60 ambapo litagharimu takribani Sh. bilioni 5.6 hadi kukamilika kwa mchakato huo mzima wa ujenzi wa awali.

‘’Kukamalika kwa maradi huu tunatarajia sasa kwa mkoa huu wa mtwara na ukanda mzima wa kusini uchangamke zaidi kwani ajira zitakazopatiakana hapa hazitahusika tu watu wa mtwara bali hata kutoka nje ya mkoa na sehemu kubwa ni akina mama na vijana na ajira zitapatikana nyingi zaidi katika eneo letu hili la maranje’

Hata hivyo amezitaja faida mbalimbali zitazotokana na kongani hiyo ikiwemo ajira za kawaida takribani 35 elfu kwa watu watapata ajira za moja kwa moja, uuzaji wa korosho na bidhaa zake badala ya kuuza tu korosho ghafi kama vile ganda lenyewe.

Hata hivo mafuta yanayotokana na ganda la korosho na zingine ‘’Kwahiyo mkulima ataenda kunufaika na zao lake mara mbili ya kile anachokipata na serikali itapata mapato ya kutosha kwasababu ile tozo aliyokuwa anaipata kwenye korosho ghafi sasa itapata mapato yanayozalishwa na viwanda’’

Katika hatua nyingine Naibu Katibu Mkuu huyo, ametembelea katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Nchini (TARI) Naliendele na akiwa katika taasisi hiyo amesema hadi kufikia mwaka 2050 nchi iweze kufikia uchumi wa kati wa juu na ili kufikia hapo moja ya sekta ya mageuzi ikiwemo sekta ya kilimo.

‘’Ili ufanikiwe kwenye kilimo, hakuna kilimo bila utafiti kwahiyo TARI mtakuwa sehemu kubwa muhimu ya mageuzi ya nchi hii kiuchumi kupitia utafiti na serikali imeahinisha mazao kumi na tano na korosho ni miongoni mwa mazao hayo, tunataka tufikie uzalishaji wa tani milioni 1 ifikapo 2030 na TARI Naliendele mna nafasi kubwa kutuangamiza au kutunyanyua’’amesema Hussein

Related Posts