Nyankumbu, Manungu Complex pamoto | Mwanaspoti

VIWANJA viwili vya Nyankumbu na Manungu Complex vinavyotumiwa na Geita Gold na Mtibwa Sugar vimekuwa ni mwiba mkali kwa wapinzani wanaotembelea hapo, kwani hadi sasa timu hizo hazijapoteza mchezo wowote nyumbani.

Timu hizo zilizoshuka daraja msimu uliopita, zimeendelea kuonyesha umwamba zikicheza nyumbani, Geita Gold ikicheza michezo 11, imeshinda 10 na kutoka sare mmoja, huku safu yake ya ushambuliaji ikifunga mabao 27 na kuruhusu matatu hadi sasa.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar, hadi sasa imecheza michezo 10 nyumbani kati ya 20 msimu huu, ikishinda, huku safu yake ya ushambuliaji ikifunga jumla ya mabao 23 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara mbili.

Timu nyingine zinazofuatia kwa kushinda michezo mingi nyumbani ni Stand United iliyoshinda tisa, Mbeya City na TMA ya jijini Arusha zimeshinda saba kila mmoja, huku Mbeya Kwanza na Bigman FC zikishinda sita.

Wakizungumzia hayo, Kocha wa Geita Gold, Mohamed Muya alisema siri kubwa ni malengo waliyojiwekea ya kutodondosha pointi nyumbani, huku Kocha wa Mtibwa Sugar, Awadh Juma ‘Maniche’, akisema ubora wa wachezaji unachangia mwenendo mzuri kwao.

Related Posts