Mamia ya askari wa Jeshi la Polisi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wanadaiwa kujiunga na waasi wa M23 katika Mji wa Bukavu baada ya kuuteka mji huo.
Waasi wa M23 waliingia Bukavu wiki iliyopita na kufanikiwa kuuteka mji huo ambapo majeshi ya serikali yalitoweka kimyakimya na kuwafanya waasi hao waushikilie mji huo, ukiwa ni wa pili baada ya Goma.
Inaelezwa kuwa takribani polisi 1,800 wamejisalimisha kwa M23 huku wengine 500 wakitarajiwa kujisalimisha ambapo wanaenda kupewa mafunzo ya itikadi za M23.