WANANCHI LINDI WAENDELEA KUNUFAIKA NA ZIARA YA KATA KWA KATA YA MKUU WA WILAYA

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe Victoria Mwanziva anaendelea na ziara maalum ya kata kwa kata kwa malengo ya ukaguzi wa miradi sambamba na kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali za wananchi.

Aidha, Ziara hiyo imeifikia Kata ya Mipingo na kata ya Kitomanga katika Jimbo la Mchinga, Manispaa ya Lindi. DC Lindi amefanya ukaguzi na uwekaji jiwe la msingi Ujenzi wa Zahanati ya Namkongo- Kijiji cha Namkongo; Kata ya Mipingo.

Sambamba na hilo amefanya Ukaguzi wa Bwalo la Chakula, Madarasa, Vyoo na Mabweni ya Shule ya Sekondari Mipingo- Kijiji cha Mipingo, Kata ya Mipingo ikiwa Shule hii imepokea zaidi ya Milioni 450 kwa ajili ya maboresho ya miundombinu na ni moja kati ya shule zinazofanya vizuri sana kitaaluma Manispaa ya Lindi.

Katika hatua nyingine, Mhe Victoria ameshiriki Mkutano wa Chama Cha Msingi Pachani- Kijiji cha Mkwajuni, Kata ya Kitomanga na kutoa ujumbe wa maboresho makubwa ya huduma za Ugani haswa kwa kupata ma-Afisa ugani makhususi wa zao la Korosho ambapo pia amegusia suala la maboresho katika kupatikana viwatilifu kwa ruzuku ya Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan aliyelenga kuwekeza kwenye kilimo ili kiinue Uchumi wa Taifa letu.

Mwisho DC Mwanziva amehitimisha ziara hii kwa kufanya Mkutano wa Hadhara na Wananchi- Kijiji cha Namkongo- ambapo amesikiliza na kutatua changamoto mbalimbali- Moja ya changamoto kuu ikiwa ni barabara na kuwapatia Taarifa wananchi wa Mipingo kuwa Tarura imetenga Bajeti kwa Mwaka wa 2025/2026 kugusa maeneo korofi katika Kata ya Mipingo ili kurahisisha usafirishaji kiujumla. 



Related Posts