Dar es Salaam. Mrufani, Salum Bakari Malunge (70) aliyevaa kofia, anayetumikia kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la kulawiti pamoja kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka binti mwenye umri chini ya miaka 18, akiwa ameshikwa mkono na mrufani mwenzake Isdori Mushi (55) wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati kesi zao zilipoitwa kwa ajili ya kutajwa leo Jumamosi Februari 24, 2025.
Malunge amekata rufaa Mahakama Kuu kupinga adhabu hizo mbili, ambazo alihukumiwa mwaka 2024 baada ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kumtia hatiani.
Kwa upande wake Mushi (mwenye shati jeupe), naye amekata rufaa Mahakama Kuu kupinga kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka, ambapo hukumu yake ilitolewa mwaka 2023 katika Mahakama ya Wilaya ya Temeke, baada ya kupatikana na hatia ya katika kosa hilo.
Hata hivyo kesi hizo, zitatajwa tena Mahakama Kuu, itakayoketi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Machi 5, 2025.
Endelea kufuatilia Mwananchi.