AGIZO LA RAIS SAMIA LA KUFUNGUA VIWANDA VYA TEHAMA NCHINI LAFANIKIWA ARUSHA.

Na Pamela Mollel,Arusha

Baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuagiza Tume ya Tehama Nchini kawatafuta wawekezaji watakao fungua viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali za Tehama,agizo hilo limefanikiwa kwa kuwepo kwa kiwanda cha uzalishaji wa bidhaa za Tehama hapa Nchini

Akizungumza jijini Arusha mara baada ya kutembelea kiwanda cha Tanztech Electronics Limited kilichopo jijini Arusha,Mkurugenzi Mkuu,Tume ya Tehama Dkt Nkundwe Mwasaga anasema uwepo wa kiwanda hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa bidhaa za Tehama zitakazosaidia kukua kwa uchumi wa kidigitali

“Rais Samia alituagiza kutafuta wawekezaji ambao watafungua viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali za Tehama “Anasema Dkt Mwasaga

Anasema kuwa mwekezaji wa kiwanda hicho ameitikia wito wa Mh.Rais wa kuhakikisha Tanzania inapiga hatua katika bidhaa za Tehama

“Uwepo wa kiwanda hichi kitasaidia upatikanaji wa vifaa vya Teknolojia ikiwemo kompyuta mpakato,simu za mkononi pamoja na vifaa vingine “Anasema Dkt Mwasaga

Ameongeza kuwa kazi yao kama Tume ya Tehama ni kuhakikisha wanakuza uchumi wa kidigitali huku wakisimamia viwanda kukua

“Takwimu za hivi karibu kutoka Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA)inaonyesha simu janja zipo milioni 23 hivyo hii ni fursa katika soko”Anasema Dkt Mwasaga

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hiyo Gurveer Hans anasema changamoto kubwa katika uendeshaji ni uwepo wa kodi kubwa wanaotozwa katika uzalishaji hadi usambazaji wa bidhaa

Aidha ameomba serikali kupunguza kodi ili kuweza kuuza bidhaa kwa bei nafuu ili kila Mtanzania aweze kumudu kununua bidhaa hizo zinazotengenezwa Tanzania

 

Related Posts