Benki ya CRDB yakabidhi vitendea kazi kurahisisha kuwezesha mikopo ya 10%

Katika hatua ya kuboresha utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri, Benki ya CRDB leo imekabidhi vitendea kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 45 kwa maafisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya jiji la Dar es Salaam.

Msaada huo umekabidhiwa mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo kwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa katika hafla ya utambulisho wa taasisi za fedha zilizopewa dhamana ya usiamamizi wa mikopo hiyo ya asilimia 10 katika halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.

Benki hiyo inajivunia kuwa mshirika wa Serikali katika kusimamia utekelezaji wa mpango mpya wa uwezeshaji wa wajasiriamali wanawake, vijana, na makundi maalum kupitia mikopo ya asilimia 10 ya halmashauri.

Benki ya CRDB imekuwa kinara katika utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali nchini, ambapo asilimia 30 ya mikopo yetu inawalenga wajasiriamali wadogo. Aidha, kupitia programu ya IMBEJU, inayoendeshwa na CRDB Bank Foundation, tumewafikia zaidi ya wajasiriamali 800,000 tangu 2023, huku mitaji wezeshi ya zaidi ya Shilingi bilioni 20.2 ikitolewa.










Related Posts