Dkt. Samia Aweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Umwagiliaji la Mkomazi korogwe,

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweka Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Umwagiliaji la Mkomazi lililopo wilayani korogwe, mkoani Tanga tarehe 24 Februari 2025 na kuzungumza na wananchi ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani humo.
Amesema Dhamira ya Serikali ni kumuinua mkulima kwa kuongeza tija kwenye Sekta ya Kilimo ambapo mradi wa mkomazi wakulima watalima na kulima mara mbili hadi mara tatu kwa mwaka bila kutegemea mvua.
Bwawa la Mkomazi litakuwa na tuta la kuzuia maji lenye urefu wa zaidi ya mita 300 na barabara za mashambani zaidi ya kilomita 56, na endapo ujenzi wake ukikamilika litakuwa na lita bilioni 17 za maji ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu shilingi bilioni 48 na utanufaisha zaidi ya kata 20.
Akielezea kuhusu mradi huo, Mhe. Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo amesema kuwa jitihada za Serikali kwa nyakati tofauti za kuliendeleza bwawa hilo zimekuwa zikigonga mwamba kutokana na sabahu lukuki zikiwemo za kisiasa na kifedha lakini Serikali ya Awamu ya Sita imejidhatiti katika kuanza ujenzi huo utakaoleta tija kwa wakulima. Ameongeza kuwa Serikali inalenga kuwavutia wawekezaji wakubwa wa mazao mengine kama vile kilimo cha chai, ili kutoa fursa kwa wakulima kupata nafasi ya kuuza mazao yao kwenye soko la ndani na nje ya nchi.

Related Posts