Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Mhe. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ambaye pia ni
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, leo ametembelea Chuo Kikuu cha
Dodoma, na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Chuo.
Mhe.
Stergomena alipokelewa na mwenyeji wake Makamu Mkuu wa Chuo Prof. Lughano
Kusiluka, aliyeambatana na Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Bi. Suzan P.
Mlawi, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma Prof. Razack Lokina
na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Winester
Anderson.
Mhe.
Stergomena Tax amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Menejimenti ya Chuo katika
kusimamia ubora wa taaluma, kutunza taswira ya chuo na kuweka msisitizo wa
kuendelea kutatua changamoto zote kwa wakati, husani zile zinazohusiana na
maendeleo ya wanafunzi.
Naye
Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka, akimkaribisha Mkuu wa Chuo,
amemwelezea mikakati ya namna Menejimenti ilivyojipanga kuendelea kusimamia
ubora wa taaluma inayotolewa na Chuo, pamoja na kutoa taarifa sahihi na kwa
wakati kwa masuala ambayo yanahitaji ufafanuzi kwa jamii.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha
Dodoma, Mhe. Stergomena Lawrence Tax (Mb), ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na
Jeshi la Kujenga Taifa, akisaini kitabu cha wageni, ofisi ya Makamu Mkuu wa
Chuo, Jengo la Benjamin Mkapa, Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la
Chuo, Bi. Suzan P. Mlawi (wa kwanza kushoto) wakizungumza jambo na Mkuu wa Chuo
na viongozi wajuu wa Chuo kikuu cha Dodoma wakati wa ziara iliyofanyika jengo
la Benjamin Mkapa Dodoma.
Mkuu wa Chuo akiwa kwenye
picha ya pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dodoma.
Wajumbe wa Menejimenti ya
Chuo wakiwa kwenye Mkutano na Mkuu wa Chuo alipofanya ziara leo.

Mipango, Fedha na Utawala, Prof. Winester Anderson, akimsikiliza kwa makini
Mkuu wa Chuo.
Makamu Mkuu wa Chuo, Prof. Lughano Kusiluka (wa
kwanza kulia) akiwa na Prof. Razack
Lokina( wa kwanza kushoto), Naibu Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia Taaluma;
wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Chuo alipotembelea Utawala Mkuu leo.