Hizi ndio ‘couple’ zilizovunja rekodi ya dunia kwa kuishi muda mrefu

Ndoa ni taasisi ya kijamii inayounganisha watu wawili katika uhusiano wa karibu unaotambulika kisheria na kijamii, pia hutarajiwa kudumu kwa muda mrefu hadi kifo kitakapowatenganisha.

Hata hivyo siyo wote hufanikiwa kutimiza agano hilo takatifu kutokana na sababu mbalimbali, baadhi ya ndoa huvunjika baada ya kupita muda fulani.

Hata hivyo, imekuwa tofauti kwa wanaondoa hawa ambao kwa nyakati tofauti wamefanikiwa kuvunja rekodi ya dunia ya Guinness kwa kuishi pamoja kwa muda mrefu ndani ya ndoa.

Manoel Angelim Dino na Maria de Sousa Dino

Hawa ndio wanaoshikilia rekodi ya wanandoa walio hai ambao wameishi pamoja kwa muda mrefu kwa sasa, kwa mujibu wa tovuti ya Guinness Word Record 

Wawili hao ambao ni raia wa Brazil wamefanikiwa kuishi pamoja katika ndoa kwa miaka takriban 84 tangu walipofunga ndoa mwaka 1940.

Manoel Angelim Dino na Maria de Sousa Dino

Kwa mara ya kwanza walikutana mwaka 1936 katika mashamba ya familia, waliokwenda kwa ajili ya shughuli za kilimo na baada ya miaka kadhaa kupita walianzisha mahusiano hadi kufikia kufunga ndoa.

Kwa Manoel haikuwa rahisi kumpata Maria kwani alikumbana na kikwazo kutoka kwa familia ya mlimbwende huyo.

Awali mama yake Maria hakubariki mahusiano hayo, hivyo ilimlazimu Manoel kufanya jitihada za kuiaminisha familia hiyo kuwa ana mapenzi ya dhati na mtoto wao na ana uwezo wa kumuhudumia, pindi watakapoanzisha familia pamoja.

Alianza kwa kujenga nyumba ambayo waliitumia kuanzisha familia na Maria baada ya kuoana.

Vilevile alijishughulisha na kilimo ambacho kilimsaidia kupata kipato kwa ajili ya kuihudumia familia yake.

Kwa pamoja wameweza kubarikiwa kupata watoto 13, wajukuu 55, vitukuu 54 na vilembwe 12 na Kwa sasa Manoel amefikisha umri wa miaka 105 na Maria 101.

Katika mahojiano yao na tovuti ya Word Guiness Record, Maria alisema siri iliyowawezesha kuishi pamoja kwa muda mrefu ni upendo.

“Upendo wa dhati ndio uliotuwezesha sisi kufika hapa, upendo ambao hata kompyuta ya kisasa haiwezi kuuhesabu wala kuufafanua” alieleza Maria.

Herbert na Zelmyra Fisher

Wanandoa hawa ambao ni raia wa Marekani walifanikiwa kuishi pamoja kwa takriban miaka 86 hadi pale Herbert Fisher alipoaga dunia Februari 27, 2011.

Kwa mujibu wa tovuti ya Guinness Word Record wawili hao walizaliwa na kulelewa katika eneo moja huko Kaskazini mwa jimbo la Calfonia nchini Marekani.

Herbert na Zelmyra Fisher

Walianza kwa kuwa marafiki ambao kwa lugha ya sasa ya vijana wanaitana ‘BFF’ hadi walipofunga ndoa Mei 13, 1924, Herbert akiwa na umri wa miaka 18 wakati Zelmyra akiwa na miaka 16.

Kwenye moja ya mdahalo uliofanyika katika maadhimisho ya siku ya wapendanao (Valentine Day) mwaka 2010 kupitia mtandao wa Twitter (kwa wakati huo sasa X) wawili hao walibainisha siri ya uhusiano wao kudumu kwa muda mrefu.

Katika mdahalo huo walisema siri yao kubwa ni urafiki walioujenga baina yao ambao unasababisha upendo walionao kuimarika kila siku.

“Hatujawahi hata kufikiria kuwa talaka inaweza kuwa suluhu ya changamoto yeyote tuliowahi kupitia”walieleza.

Kwa muda wote walioishi wawili hao walibahatika kupata watoto watano, wajukuu 10, vitukuu tisa na kilembwe mmoja.

Wawili hao walifanikiwa kuishi pamoja katika ndoa kwa takriban miaka 81 baada ya kufunga ndoa Mei 25, 1940.

Mwaka 2021 wawili hawa walipatiwa tuzo na Guinness Word Record kuwatambua kama wanandoa walio hai ambao wameishi kwa muda mrefu pamoja.

Wanasisitiza kuwa uimara wa ndoa yao waliujenga katika misingi ya upendo, ukweli, kuoneana huruma pamoja na kushirikiana.

Siri kuishi katika ndoa kwa muda mrefu

Kwa mujibu wa tovuti ya Marriage.com ndoa ili iweze kudumu kwa muda mrefu inatakiwa kujengwa katika misingi ya upendo, uvumilivu, heshima, kusameheana na uaminifu.

Imeandikwa na Mariam Mbwana na Mashirika

Related Posts