Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Hawa Hussein Ibrahim, maarufu kama Carina, ameondoka leo kuelekea India kwa ajili ya matibabu baada ya kukamilika kwa taratibu za safari na gharama za matibabu.
Kabla hajaondoka, akiwa nyumbani kwao na akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Carina amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na taasisi na watu mbalimbali waliomsaidia, hususan Sheikh Suleiman na Watanzania waliochangia kufanikisha safari yake.
Jumla ya michango iliyopatikana inakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 54.
Katika safari yake, Carina ameacha ujumbe maalum kwa familia yake, akiwatakia kheri na kuwaombea watoto wake pamoja na mama mzazi.
Kwa muda wa miaka tisa, muigizaji huyo amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya tumbo na kufanyiwa upasuaji zaidi ya mara 24. Sasa, matumaini ya kupata nafuu yapo mbele yake baada ya kusafiri kwenda kupatiwa matibabu maalum nchini India