WAZIRI GWAJIMA ATETA NA KAMATI MAANDALIZI YA SIKU YA WANAWAKE KITAIFA MKOANI ARUSHA.

Na Jane Edward, Arusha 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi maalum, Dkt. Doroth Gwajima ameupongeza Mkoa wa Arusha kwa maandalizi mazuri kuelekea wiki ya wanawake duniani, akihimiza jitihada zaidi kwenye utekelezaji wa mikakati ya kuwainua wanawake katika nyanja mbalimbali pamoja na kuondoa unyanyasaji na ukatili wa aina mbalimbali kwa wanawake na wasichana.

Gwajima ameyasema hayo wakati  akizungumza na wajumbe wa kamati mbalimbali za maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani Machi 08, 2025, 

Amesisitiza pia umuhimu wa Mkoa wa Arusha na mikoa mingine kote nchini, kuendelea kutoa elimu ya afya, Mikopo kwa wanawake sambamba na kuwafahamisha wananchi kuhusu fursa za uwezeshaji wanawake kiuchumi.

Akikemea udhalilishaji na ukatili wa kijinsia unaotokana na baadhi ya tamaduni katika Mikoa ya Arusha na Manyara inayopelekea ukeketaji kwa wasichana, Dkt. Gwajima amesema umuhimu wa kubuniwa mikakati mbalimbali ya kutokomeza ukatili huo ili kubadilisha sura na takwimu za unyanyasaji katika Mikoa hiyo pamoja na kutokomeza fikra na tamaduni za kale zisizokuwa na faida kwa zama hizi.

Hata hivyo wadau mbalimbali walihudhuria kikao hicho ikiwemo washauri wa Rais Mhe. Angellah Kairuki pamoja na Mhe. Sophia Mjema, Katibu tawala Mkoa wa Arusha Musa Missaile, wadau mbalimbali kutoka Taasisi za kifedha zikiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation Tully Mwambapa 

Related Posts