WAZIRI KIKWETE- “TUNDUMA WAMETEKELEZA MAAGIZO YA RAIS SAMIA KWA KUTOA BIL 4.6 MIKOPO YA 10%"

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete amesema hatua ya Halmashauri ya Tunduma kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 4.6 kwa vikundi 150, ikiwa ni mikopo ya Halmashauri ya asilimia 10 itokanayo na mapato ya ndani kwa ajili ya vikundi vya wananwake, vijana na watu wenye Ulemavu ni utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyeelekeza Halmashauri zote nchini kuanza kutoa mikopo hiyo kwa kutumia mfumo mpya wa utoaji na usimamizi wa mikopo hiyo.

Akiongea leo tarehe 25 Februari 2025 wakati akikagua miradi ya maendeleo mkoani Songwe, Mhe. Kikwete amebainisha kuwa katika kuhakikisha mikopo hiyo inakuwa na tija kwa Walengwa Mhe. Rais Samia alielekeza kupitia na kuboresha utoaji wa mikopo hiyo ambapo baada ya kukamilika maboresho hayo, dirisha la utoaji mikopo lilifunguliwa rasmi mwezi Septemba 2024.

Aidha, amesema katika uongozi wa Mhe.Rais Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake amejitahidi kuhakikisha vijana wanafunguliwa fursa na kuwezeshwa, maelekezo yake hayo yamekuwa yakifanyiwa kazi na Halmashauri, Serikali Kuu,hivyo amevitaka vikundi kutumia fedha hizo kwenye miradi yenye tija na kurejesha kwa wakati ili na wengine wanufaike na mikopo hiyo.

Katika hatua nyingine Mhe.Kiwete amekagua na kuweka jiwe la msingi katika miradi ya Ujenzi wa majengo ya Hospitali ya Halmashauri ya Momba,

Jengo la NMB na Majengo ya madarasa ya ghorofa ya shule ya sekondari Uwanjani na kikundi cha Vijana cha Ufugaji kuku Chipaka.

Mhe. Kikwete amewapongeza Wabunge wa majimbo hayo ya Momba na Tunduma, Mhe. Condester Sichwale- Momba na Mhe.David Silinde-Tunduma kwa kuhakikisha wanatafsiri maono ya Mhe. Rais Samia kwa vitendo ya kuwaletea maendeleo wananchi

Naye Mkuu wa mkoa wa Songwe, Mhe. Daniel Chongolo amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika mkoa huo hali inayo chochea mapato ambayo husaidia Halmashauri za mkoa huo kupata mapato na kuweza kutoa mikopo ya asilimia 10 kutokana na mapato ya ndani.







Related Posts