Na Khadija Kalili Michuzi TV
Msewa, Kibaha.
Msajili wa Hazina na CAG kushirikiana katika usimamizi wa Mashirika ya Umma wamekutana kwa siku mbili kujadili namna bora ya mashirika ya Umma kuboresha utendaji kazi ilikuongeza ufanisi, kuleta tija kwa Umma na kuondoka na utegemezi wa ruzuku za serikali na mashirika hayo yatoe gawio kwa serikali.
Hayo yamesemwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na kuongozwa na Msajili wa Hazina Nehemiah Mchechu wakati akifunga Kikao kazi Cha pamoja kati ya Ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG na Ofisi ya Msajili wa Hazina na Ofisi ya taifa ya Ukaguzi Cha siku mbili katika ukumbi wa Shule ya uongozi ya Mwalimu Nyerere Kibaha.
Amesema kikao kazi hicho cha kwanza cha pamoja ambapo wamekubaliana kukutana Kila mwaka ili kujadili mikakati ya pamoja ya uboreshaji wa usimamizi wa taasisi za Umma na kuweka mikakati ya mashirika ya Umma yawe na tija kwa taifa.
Katika kikao hicho kilichoratibiwa, pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bw. Charles Kichere, pande mbili hizo zilijadili juu ya haja ya taasisi za umma kukumbatia utendaji unaozingatia sheria, matumizi ya TEHAMA, na mafunzo kwa watumishi yote haya yakilenga uimarishaji wa taasisi na mashirika ya umma.
Msajili wa Hazina Bw. Nehemiah Mchechu, alisema ili serikali ifanikiwe katika mageuzi inayofanya kwenye taasisi za umma, suala la utawala bora halikwepeki.
“Lazima tuboreshe utawala bora na ndio maana tumeona haja ya kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ambayo ndio yenye jukumu kubwa la kuhakikisha kunakuwa na utawala bora katika taasisi za umma,” alisema Mchechu.
“Kwa pamoja tumekubaliana kuboresha uhusiano wa kiutendaji kati ya taasisi hizi mbili za serikali. Katika hili tumeona haja ya kuwa na muingiliano “interaction” wa mara kwa mara kati ya menejimenti ya Ofisi hizi mbili. Kwa kufanya hivyo, Bw. Mchechu alisema ufanisi wa taasisi za umma utaongezeka na hivyo kuongeza mchango wao kwenye mfuko mkuu wa Serikali.
“Tayari kuna tija nzuri, lakini shauku yetu ni kuona taasisi hizi za umma zinaongeza ubunifu na ufanisi ili tupate matokeo chanya ya uwekezaji unaofanywa na Serikali,” alisema.
Kwa mujibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina, hadi kufikia Juni 30, 2024, Serikali ilikuwa imewekeza kiasi cha Sh 86.3 trilioni katika taasisi 308 ambazo inazisimamia, ikiwemo zile ambazo ina hisa chache. Kiasi hicho ni ongezeko la asilimia 14.2 ikilinganishwa na Sh75.6 trilioni, kiasi kilichowekezwa hadi kufikia mwaka 2023.
Lengo la Serikali ni kuona Taifa na watanzania kwa ujumla wananufaika na uwekezaji huu wa serikali na ndio maana pamoja na kuongeza uwekezaji, kuna hatua kadhaa tunazichukua ikiwemo kuweka mifumo imara ya usimamizi, uendeshaji na uwajibikaji katika taasisi za umma.
Amesema Kuna baadhi ya mashirika ya Umma ya fanyabiashara hivyo yahakikishe yanazalisha kwa ufanisi yapate faida yajiendeshe na yatoe gawio kwa serikali badala ya kusubiria Ruzuku za serikali kujiendesha.ambazo
“Kuna haja ya baadhi ya mashirika ya Umma kupunguza utegemezi wa ruzuku ya serikali kwa kubadilika kutoka taasisi za kutegemea serikali badala yake wawe wanatoa gawio kwa serikali baada ya kuwa wametengeneza faida badala ya mashirika hayo kwenda tena kuchukua Ruzuku” alisema CPA Kichere.
Kikao kazi hiki tumetathimini kwa pamoja mbinu ambazo zinaweza kuleta mabadiliko chanya katika kusimamis na kuendeleza mashirika hayo na kutafutia mbinu za kutatua mapungufu mbalimbali ikiwemo kukosekana kwa ufanisi wa uthibiti na ufanisi na kuwepo kwa mianya na upotevu wa mapato ya serikali, ukosefu wa ajira na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.
Alisema mashirika ya Umma ni nguzo muhimu ya kutatua changamoto mbalimbali zinazozikabili masuirika ya uuma nchini na taifa kwa kwa kujadili na kutathimini mbinu zinaze
Wananchi ikiwa ni sehemu ya dhamira na jitihada za kuhakikisha taasisi na mashirika ya umma yanaongeza mchango katika ustawi wa uchumi wa Taifa, Ofisi ya Msajili wa Hazina na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi zimekubaliana kushirikiana katika maeneo nane ya kiusimamizi.
Ametaja maeneo waliyokubaliana kushirikiana ni utawala bora, ufanikishaji wa utekelezwaji wa mapendekezo ya ukaguzi, kuboresha mifumo ya usimamizi na uongozi, usimamizi mzuri wa rasilimali za umma, uwajibikaji wa kifedha., kutekeleza kwa vitendo na kuiishi falsafa ya R 4 za Mhe. Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG CPA Charles Kichere alisema kikao cha Ofisi yake na Ofisi ya Msajili wa Hazina kilikuwa na tija kwani walijadili mambo muhimu yanayogusa maslahi ya Taifa.“Tulijadili kuhusu kuboresha uwajibikaji wa kifedha na utekelezaji wa maazimio mbalimbali yanayolenga kuhakikisha kuwa fedha za umma zinatumika kwa ufanisi, uwazi na kwa kuzingatia misingi ya utawala bora,” alisema Kichere.
Pia katika Mkutano wa Ofisi hizo mbili walikubaliana kushirikiana linapokuja suala la kuhakikisha taasisi za umma zinatekeleza mapendekezo ya ukaguzi “Audit recommendations”.
“Katika hili Msajili wa Hazina peke yake hawezi, halikadhalika Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali na ndio maana tumeona haja ya kuzungumza lugha moja,” alisema Kichere.
Pia, katika orodha ya maeneo ya ushirikiano ni juu ya namna bora ya kuhakikisha taasisi za umma zinasimamia vizuri rasilimali za umma ili zijiendeshe kwa ufanisi na hivyo kupunguza utegemezi kutoka serikali kuu.
“Tunataka kuona mashirika ya umma yanapunguza utegemezi na badala yake yawe mstari wa mbele katika kutunisha mfuko wa serikali kuu,” alisema Kichere.
Ili kuongeza ufanisi, Bw. Kichere pia alisema Ofisi yake na ya Msajili wa Hazina walikubaliana kutengeneza mazingira ya taasisi za umma kukumbatia matumizi ya TEHAMA pamoja na mafunzo kwa watumishi.
“Lazima tuwajengee uwezo watumishi wa mashirika ya umma na pia hatuna budi kukumbatia matumizi ya TEHAMA ikiwa tunataka kuongeza ufanisi,” alisema.Bw. Kichere
Aliongeza kuwa “Tuko tayari kuendelea kubadilishana mawazo na uzoefu na Ofisi ya Msajili wa Hazina ili serikali ifikie malengo yake ya kuboresha mashirika ya umma.”