RAIS SAMIA ATOA SHILINGI MILIONI 60 KUMALIZA KERO YA MAJI SAFI NA SALAMA KWA WAKAZI WA KIJIJI CHA KIMBANGA

Na Mwandishi Wetu,Nyasa


RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan,amerudisha matumaini  kwa wananchi  wa
kijiji cha Kimbanga Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma,baada ya kutoa  kiasi
cha Sh.milioni 60 kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji ili kumaliza
kero ya huduma ya maji safi na salama iliyokuwepo kwa muda mrefu  katika
kijiji hicho.


Kwa sasa,wakazi wa kijiji cha Kimbanga wanatembea umbali wa kilometa 1
hadi 2 kila siku kwenda vijiji vya jirani kutafuta maji,jambo
linalowarudisha nyuma kimaendeleo licha ya kuwa wakulima wazuri wa mazao
ya chakula na biashara ikiwemo zao maarufu la Kahawa.


Akizungumza na wakazi wa kijiji hicho Kaimu Meneja wa Ruwasa Wilayani
Nyasa Athuman Chola alisema,Ruwasa Wilaya ya Nyasa imepokea Sh.milioni
300 zilizoletwa na Rais Samia Suluhu Hassan ili kuchimba visima vya maji
katika vijiji vitano ikiwemo kijiji cha Kimbanga.


Alisema,katika kijiji cha Kimbanga kazi ya kuchimba kisima imekamilika
na sasa wanaendelea kujenga kioski cha kuchotea maji ambacho ujenzi wake
umefikia asilimia zaidi ya 40.


Chalo ametaja kazi ya zilizobaki ni kusambaza  mabomba ya maji kwenda
kwenye makazi ya Wananchi,kujenga vituo vya kuchotea,kufunga mashine ya
kusukuma maji kutoka kwenye kisima na kupeleka kwenye tenki na kufunga
umeme jua.


“mpaka sasa tumefanikiwa kuchimba kisima katika Kijiji cha Kimbanga
pekee na kwenye vijiji vinne tumeshindwa kupata maji chini ya ardhi,hata
hivyo tutatumia njia mbadala ikiwemo kuboresha chamchem na kujenga
miradi ya mserereko  kwa kutoa maji milimani na kupeleka kwa
wananchi”alisema Chola.


Aidha alisema,katika kijiji cha Malamala wanaendelea kufanya usanifu
upya kwani imeshindikana kupata chanzo cha maji cha uhakika na
watashirikiana na mamlaka  ya Bonde la Ziwa Nyasa ili wananchi waweze
kupata maji ya uhakika.


Ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan,kwa kutenga fedha ili kutekeleza miradi ya maji katika
vijiji mbalimbali ambayo  inalenga kupunguza na kumaliza kabisa
changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi.


Baadhi ya Wakazi wa kijiji cha Kimbanga,wameishukuru Serikali  kupitia
Wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini(Ruwasa)kwa uamuzi wa
kutatua changamoto ya maji safi na salama katika kijiji chao.


Adelius Mwingira alisema,mradi wa kisima utasaidia kuwaondolea kero ya
muda mrefu ya kutumia maji  ya visima vya asili ambavyo maji yake siyo
safi na salama pamoja na mateso ya kubeba ndoo za maji  kichwani kila
siku.


Bonus Kapinga alisema,mradi wa kisima ni ukombozi mkubwa kwao kwa sababu
kijiji hicho tangu kilipoanzishwa miaka zaidi ya 50 hakijawahi kupata
mradi wa maji ya bomba badala yake wanatumia maji kutoka vyanzo vingine
vya asili kama mito na mabonde yanayop kando kando ya kijiji hicho.


Alisema,kero hiyo inasababisha hata  maendeleo ya kitaalum kwa wanafunzi
wa shule ya msingi kuwa chini kwa kuwa muda wa masomo wanafunzi
wanakutumia kwenda kutafuta maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali.


William Komba,ameishukuru Serikali kupeleka mradi wa kisima cha
maji,lakini ameiomba Serikali kupitia Ruwasa kuhakikisha inakamilisha
ujenzi wa  kisima hiko haraka na kufikisha mtandao wa maji kwenye makazi
ya wananchi ili wasiendele kuteseka kwa kutembea umbali mrefu hadi
kwenye vituo vya kuchotea maji.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa kioski cha kuchotea
maji katika kijiji cha Kimbanga Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma kupitia
mradi wa uchimbaji visima 900/5 kwa kila Jimbo ambapo Wilaya ya Nyasa
imepata visima vitano vitakavyochimbwa kwa gharama ya Sh.milioni 300.

 

Related Posts