Fanya haya kuepuka ‘mood swings’ kwa wenye kisukari

Watu wengi wanaoishi na kisukari hukumbana na tatizo la mabadiliko ya ghafla ya kihisia, maarufu kama ‘mood swings’.

Hali hii inaweza kuleta athari si tu kwa afya zao kwa ujumla bali hata katika uhusiano wao wa kijamii na utendaji wa kila siku.

Hali ya sukari inashuka chini ya kiwango cha kawaida na hivyo  kumsababisha mtu kuhisi wasiwasi, hasira, kuchanganyikiwa au hata kupata hali ya huzuni.

Ubongo unahitaji sukari ili kufanya kazi vizuri, na pindi sukari inaposhuka zaidi ya kiwango cha kawaida husababisha ubongo usifanye kazi yake na huathiri moja kwa moja hisia na utulivu wa mtu.

Kupanda kwa sukari mara kwa kwa mara kunaweza kusababisha uchovu, kukosa uvumilivu, na hata hisia za huzuni au msongo wa mawazo hivyo kufanya wenye kisukari awe na mabadiliko ya hisia kila mara.

Msongo wa mawazo, kuishi na kisukari kunahitaji uangalizi wa hali ya juu, ikiwa ni pamoja na kupima sukari mara kwa mara, kuchagua mlo sahihi, na kutumia dawa kwa wakati.

Hili linaweza kuwa mzigo mkubwa kiakili na kihisia, na kusababisha mtu kuhisi kuchoka, kukata tamaa au kuwa na hasira mara kwa mara.

Mabadiliko ya homoni kama adrenaline, cortisol, na serotonin huathiriwa na viwango vya sukari kwenye damu. Wakati sukari inashuka au kupanda kwa ghafla, homoni hizi zinaweza kuleta hisia za huzuni, uchovu, au hata hasira isiyoeleweka.

Watu wenye kisukari mara nyingi hukosa usingizi mzuri kutokana na sababu kama vile haja ndogo ya mara kwa mara au msongo wa mawazo kuhusu kudhibiti sukari. Ukosefu wa usingizi unaweza kuongeza hatari ya kuwa na ‘mood swings’.

Baadhi ya watu wenye kisukari hupata upungufu wa madini kama magnesium na vitamini B12, ambayo yana mchango mkubwa katika utulivu wa kihisia. Upungufu wa virutubisho hivi unaweza kusababisha uchovu wa kiakili na hisia za huzuni.

Kuepuka hali ya mabadiliko ya kihisia ni muhimu kwa wetu wenye kisukari kufuata mpangilio sahihi wa lishe.

 Kula mlo wenye uwiano mzuri wa virutubisho, kula kwa wakati kunaweza kusaidia kudhibiti viwango vya sukari.

Kufuatilia na kupima viwango vya sukari mara kwa mara husaidia kuchukua hatua mapema kabla ya hali kuwa mbaya.

Mazoezi husaidia mwili kudhibiti sukari na huongeza utolewaji wa homoni za furaha kama endorphins, ambazo hupunguza msongo wa mawazo na kuboresha hali ya hisia.

Pata usingizi wa kutosha, kulala  kwa saa 7-9 kwa usiku ni muhimu kwa utulivu wa kihisia. Ni vyema kuepuka matumizi ya vinywaji vyenye kafeini au kutumia simu kabla ya kulala ili kusaidia kupata usingizi mzuri.

Related Posts