Na Mwamvua Mwinyi, Pwani Februari 28,2025
Huo ni utambuzi wa kipekee kwa mkoa huo, na ni fursa muhimu ya kukuza maendeleo katika nyanja mbalimbali, ikiwemo uchumi, utalii na huduma za kijamii.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Alhaj Abubakari Kunenge, aliwataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uzinduzi wa tukio hili la kihistoria.
Akizungumza na waandishi wa habari, RC Kunenge alisema, “Ni heshima kubwa kwa Mkoa wetu kuwa mwenyeji wa tukio hili, ambalo litakusanya viongozi wa kitaifa, mikoa ya jirani, na wananchi wa Mkoa wetu kwa pamoja.”
Alhaj Kunenge alikumbusha kuwa wakati wa maadhimisho ya kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya Baba wa Taifa mwaka 2024, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan alitangaza kuwa uzinduzi wa Mwenge wa Uhuru 2025 utafunguliwa rasmi katika Mkoa wa Pwani.
“Sherehe za uzinduzi zitapambwa na matukio mengi ya kupendeza, ikiwemo halaiki na burudani kutoka kwa wasanii maarufu wa nchini, ambapo Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru 2025 ni “Jitokeze Kushiriki Uchaguzi Mkuu wa 2025 Kwa Utulivu na Amani”, inayolenga kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi kwa utulivu, mshikamano na uzalendo ili kudumisha amani na maendeleo ya taifa .
Mwenge wa Uhuru ni alama ya maendeleo, mshikamano na amani, na hivyo ni muhimu kwa wote kushiriki kwa pamoja katika tukio hili la kihistoria.
Baada ya uzinduzi, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa katika halmashauri zote tisa za Mkoa wa Pwani,ikiwa ni sanjali na kutembelea ,kuzindua na kuweka mawe ya msingi miradi maendeleo.