Kula matunda haya kuboresha afya ya ubongo wako

Dar es Salaam.Kumbukumbu ni kipengele muhimu cha afya ya akili kinachohusiana na uwezo wetu wa kujifunza, kutunza kumbukumbu na kufanya uamuzi wa kila siku.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa uwezo huo hupungua kadri umri  wa mtu unavyozidi kuwa mkubwa.

 Hata  hivyo,  aina mbalimbali za utafiti wa kisayansi zimeonyesha kuwa baadhi ya matunda yana faida kubwa katika kuboresha afya ya kwa kuongeza uwezo wa kumbukumbu.

Matunda yanayotajwa ni yale yenye virutubisho muhimu,  antioxidants (vilinda seli mwilini),vitamini na madini ambayo husaidia kupigana na uharibifu wa seli za ubongo na kuboresha mtiririko wa damu kwenye ubongo ili kuongeza ufanisi wa kiakili

Inaelezwa kwa mujibu wa utafiti, matunda jamii ya michungwa, komamanga, ndizi, tufaha, zabibu, parachichi,   ni miongoni mwa matunda yaliyothibitishwa kuongeza kumbukumbu na uwezo wa kujifunza.

 Watafiti wanasema  uwepo wa madini, kemikali na madini yaliyopo kwenye kwenye matunda hayo, hupambana na uharibifu wa ubongo na kuboresha afya ya seli za ubongo.

Aina za matunda na mchango wake kwenye ubongo

Makomamanga na zabibu: Matunda haya ni kati ya matunda bora yenyen antioxidanti na flavonoidi ambazo husaidia kupambana na  umeme wa asili katika mwili ili kupunguza uharibifu wa seli za ubongo.

Matunda jamii ya michungwa na papai: Matunda haya ni yale yenye asili ya limau, chungwa na chenza ambayo huwa na virutubisho kama vitamin C ambayo ni muhimu kwa afya ya ubongo.

Vitamin iliyoko kwenye matunda haya,  inahusishwa na kuzuia uharibifu wa seli za ubongo na kuimarisha kazi za akili kwa kutunza kumbukumbu.

Tufaha: Tunda hili ni chanzo kizuri cha kemikali yenye virutubisho vinavyo pambana na uchochezi na uharibifu wa seli za ubongo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na  Chuo Kikuu cha Harvard, kemikali hiyo hupunguza dalili za kupungua kwa kumbukumbu na kuboresha utendaji kazi wa ubongo.

Parachichi: Kadhalika tunda hili linatajwa kuwa chanzo kizuri cha kemikali ya kupambana na mafuta mwilini, ambayo husaidia kuboresha mtiririko wa damu katika ubongo na kusaidia utendaji wa seli za ubongo.

 Ndizi: Tunda hili linatajwa kuwa na vitamini B6, ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa virutubisho ambavyo vinahusiana na hali ya akili, kumbukumbu na mtindo wa kujifunza.

Related Posts