Tanga. Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir ametangaza kutoonekana kwa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, nchini na nchi jirani hivyo waumini wa dini ya Kiislam wataanza rasmi kufunga Machi 2,2025.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kuandama kwa mwezi Mtukufu wa Ramadhani leo Ijumaa Februari 28,2025 mkoani Tanga, Mufti Zubeir amesema, “kamati ya mwezi imefuatilia maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na visiwani ila hawakupata taarifa yoyote kuhusu mwandamano wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.
“Haijapatikana habari yoyote ya mwezi wa Ramadhani nchini kote kuonekana iwe kwa Tanzania bara wala visiwani, kwa ninawaarifu Watanzania kuwa tunakamilisha Mwezi Shaaban 30, hivyo tutaingia mwezi wa Ramadhani Machi 2,2025.
Waumini wa dini wa Kiislam hufunga Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ikiwa ni moja ya nguzo tano za dini hiyo.
Endelea kufuatilia Mwananchi