Rais Samia Kuzungumza Na Wananchi Mkwakwani – Global Publishers


Rais Samia Suluhu Hassan, leo Ijumaa, Februari 28, 2025, anaendelea na ziara yake mkoani Tanga katika Jimbo la Tanga Mjini, ambapo anatarajiwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara na kuzungumza na wananchi kwenye viwanja vya Mkwakwani, Jijini Tanga.

Aidha, kulingana na ratiba iliyotolewa awali na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Batilda Buriani, Rais Samia kesho Jumamosi, Machi 01, 2025, akiwa jijini Tanga, atatembelea na kukagua maboresho makubwa ya Bandari ya Tanga, ambapo takribani shilingi bilioni 429 zimetengwa kwa ajili ya kuongeza kina cha bandari hiyo ili kuruhusu meli kubwa kutia nanga.

Awali, katika ziara yake mkoani Tanga, Rais Samia akiwa Handeni alizindua Hospitali ya Wilaya hiyo, kuzindua jengo la Halmashauri ya Lushoto, kuzindua mradi wa maji Mkomazi, uzinduzi wa barabara ya Tanga – Pangani – Saadan – Bagamoyo, kuzindua Shule ya Sekondari ya Sayansi kwa Wasichana ya Beatrice Shelukindo, pamoja na kuzindua mradi wa maji Mkinga.

Rais Samia pia aliweka jiwe la msingi la upanuzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa, Pangani, na mnamo Februari 27, 2025, alikuwa mgeni rasmi katika uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa Ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa, Tanga Mjini.

Related Posts