TANZANIA YAUNGA MKONO JITIHADA ZA CTBTO KUPIGA MARUFUKU MAJARIBIO YA NYUKLIiA

Mapambano dhidi ya matumizi ya Nyuklia duniani kote
yanaendelea, huku Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi 178 zilizosaini na kuridhia
Mkataba wa Kupiga Marufuku Majaribio ya Nyuklia kati ya nchi 187 zilizotia
saini mkataba huo kwa kuzingatia athari zitokanazo na matumizi ya nyuklia kwa
watu na Dunia kwa ujumla.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Mhe. Mahmoud Thabit Kombo katika mazungumzo na waandishi wa habari kufuatia
kikao chake na Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Kupiga Marufuku
Majaribio ya Nyuklia (Comprehensive Nuclear-Test-Ban Treaty-CTBTO), Dkt. Robert
Floyd amezisihi nchi zilizosalia kuweza kutilia saini mkataba huo wenye lengo
la kulinda amani na usalama wa kila mtu duniani kote.

 

Kwa upande wake Dkt. Floyd ameipongeza Tanzania kwa kuwa
kinara katika kujenga na kuilinda amani na usalama duniani ikiwa ni pamoja na
kupinga matumizi ya nyuklia duniani.

 

“Tanzania si maneno tu bali vitendo, Tanzania haina tu
diplomasia nzuri bali ina utajiri wa ujuzi wa kisayansi na kiteknolojia. Kwa
niaba ya nchi 187 wanachama wa CTBTO shukrani kwa Tanzania kuwa na mchango
mkubwa katika amani na usalama duniani.

 

Akiwa nchini kwa ziara ya siku mbili iliyoanza Februari 27,
2025, Dkt. Floyd ametembelea atatembelea Kituo cha Ung’amuzi wa Viashiria vya
Majaribio ya Silaha za Nyuklia kilichopo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chenye
uwezo wa kung’amua viashiria vya majaribio ya silaha za nyuklia kwa njia ya
hewa na kutoa mhadhara kwa umma kuhusu “Kudumisha mafanikio ya CTBTO katika
kipindi cha mabadiliko duniani.”

 

Aidha, ametembelea ofisi za Tume ya Nguvu za Atomiki
Tanzania zilizopo Mbezi Msakuzi ambapo ameipongeza TAEC kwa kazi nzuri
wanayoifanya pamoja na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa kituo kipya cha
ung’amuzi.

Related Posts